HALI YA UTOAJI HUDUMA YA MAJISAFI, UONDOAJI MAJITAKA NA
MIPANGO ILIYOPO MKOA WA DAR ES SALAAM HADI KUFIKIA MWEZI NOVEMBA, 2017
HUDUMA YA MAJI
Huduma ya Majisafi Mkoa wa Dar es Salaam hutolewa na Mamlaka ya Maji ya Mjini Dar es Salaam (DAWASA) ambayo imekodisha shughuli za utoaji huduma kwa Kampuni ya DAWASCO kwa Mkataba wa miaka 13 (lease agreement). Maeneo yasiyohudumiwa na mtandao wa DAWASA hupata maji kutoka miradi inayoendeshwa na Taasisi, Sekta binafsi na Jumuia (COWSOs) kwa usimamizi wa Halmashauri za Manispaa na DAWASA. Chanzo kikubwa cha maji haya ni visima virefu. Hatua hizi ni za muda na dharura katika kukabiliana na uhaba wa maji. Vyanzo vikuu vya maji ni Mto Ruvu, Mto Kizinga pamoja na maji chini ya ardhi.
Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na wakazi wapatao milioni 4.5, idadi hiyo kwa mwaka 2017 inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 5.5.
Mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa mwaka 2017 ni wastani wa lita milioni 544 kwa siku ambapo uwezo wa uzalishaji ni lita milioni 504 kwa siku. Vyanzo vikuu vya maji haya ni Mto Ruvu, Mto Kizinga pamoja na maji chini ya ardhi. Maji yanayozalishwa kwa sasa yanaweza kukidhi mahitaji kwa zaidi ya asilimia 90, hali ilivyo sasa yanakidhi mahitaji kwa asilimia 72 kwa wastani wa saa 16 kwa siku. Hadi kufikia mwezi Septemba, 2017 kulikuwa na takribani visima virefu 1,171 vya jamii, visima 147 vya DAWASA na visima 600 vya Taasisi na watu binafsi. Maji yanayozalishwa na visima vya Taasisi na watu binafsi yanafikia lita za ujazo milioni 53 kwa siku ambapo yanakidhi mahitaji kwa asilimia 16.2 ya wakazi wa Mkoa. Takriban asilimia 40 ya eneo la Mkoa halina mtandao wa mabomba ya DAWASA
Kutokana na ufinyu wa mtandao, upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam hautoshelezi mahitaji, huduma ya maji hutolewa kwa maeneo yenye mtandao wa mabomba.
Maeneo machache (20%) yaliyopo hasa katika Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Ubungo hupata huduma ya maji kwa saa kati ya 20-24 wakati zaidi ya asilimia 40 hupata maji kwa mgawo wa wastani wa saa kati ya 8-16 kwa siku.
Eneo kubwa la Wilaya za Temeke na Kigamboni ndiyo yenye kiwango cha chini cha 10% cha upatikanaji wa mtandao wa mabomba. Maeneo haya yanatarajiwa kupata huduma ya maji kutoka mradi mkubwa wa DAWASA wa visima virefu 20 vya Kimbiji na Mpera.
Hadi kufikia mwezi Septemba, 2017 asilimia 72 ya wakazi waishio kwenye Mitaa katika Mkoa wa Dar es Salaam wanapata huduma ya majisafi na salama kupitia miradi ya maji iliyopo. Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kila Wilaya kwa maeneo ya vijijini ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 1.
Jedwali Na. 1: Hali ya Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini katika kila Wilaya
Na. |
Halmashauri |
Idadi ya Watu katika kila Manispaa |
Idadi ya Watu wanaopata maji katika kila Manispaa |
Idadi ya Vituo vya kuchotea maji |
Asilimia ya watu wanaopata huduma ya Maji |
1.
|
Ilala MC
|
1,527,106 |
962,077 |
1015 |
63 |
2.
|
Kigamboni MC
|
203,844 |
103,961 |
263 |
51 |
3.
|
Kinondoni MC
|
1,168,273 |
852,839 |
234 |
73 |
4.
|
Temeke MC
|
1,508,763 |
935,433 |
2,995 |
68 |
5.
|
Ubungo MC
|
1,052, 490 |
684,119 |
170 |
65 |
|
Jumla/Wastani
|
5,460,476 |
3,538,429 |
4,677 |
64 |
1.3 Hali ya Uondoshaji Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam
Mfumo (Central sewerage system) wa kuondosha majitaka uliopo Jijini Dar es salaam unahudumia asilimia 10 tu ya wakazi wote wa Jiji. Mfumo wa Katikati ya Jiji unamwaga maji baharini na mifumo mingine iko Lugalo, Chuo Kikuu cha DSM, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Kurasini, Buguruni, Uwanja wa Ndege, Airwing, Barabara ya Nyerere (Tazara), Vingunguti na Ubungo. Mifumo hii inamwaga majitaka katika mabwawa yaliyoko maeneo hayo.
Maeneo yasiyo na mfumo rasmi wanatumia vyoo vya shimo (Pit latrine) na mashimo ya choo (septic tanks) ambapo yakijaa huchukuliwa na kupelekwa kwenye mabwawa kwa ajili ya kusafisha.
Matarajio ya Mkoa ni kutoa huduma ya Majisafi na salama kwa asilimia 95 ya wakazi wa Jiji, asilimia 30 uondoshaji wa Majitaka na kupunguza upotevu wa maji kwa asilimia 25 katika Mkoa wa Dar es Salaam ifikapo 2025.
1.4.1 Mipango ya Miradi inayotekelezwa na DAWASA
Hivi sasa DAWASA wanatekeleza miradi mikubwa ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya Maji katika Mkoa wa Dar es salaam (Kiambatisho). Miradi hiyo ni pamoja na:-
Upanuzi wa Mtambo wa Ruvu Chini na ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu Chini hadi matanki ya Chuo Kikuu cha Ardhi.
Lengo la mradi huu ni kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 182 hadi 270 kwa siku. Mradi wa upanuzi wa mtambo umekamilika (100%) na umeanza kuzalisha maji mita za ujazo 270,000 kwa siku ikiwa ni ongezeko la mita za ujazo 90,000 kwa siku. Ujenzi wa bomba kuu kutoka mtambo wa Ruvu Chini lenye urefu wa kilomita 55.338 pia umekamilika (100%). Mradi huu umepunguza kero ya maji kwa wakazi wanaotumia maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini unaohusisha maeneo ya Bagamoyo na vitongoji vyake, Bunju, Mabwepande, Boko, Tegeta, Kunduchi, Mbezi Beach, Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Chuo Kikuu, Mikocheni, Msasani, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo, Mabibo, Kigogo, Buguruni, Ilala, Maeneo ya Katikati ya Jiji la DSM pamoja na Kurasini, Keko, Chang'ombe, Pugu na Bandarini.
Upanuzi wa chanzo cha Ruvu Juu na ujenzi wa bomba kuu hadi matanki ya Kibamba na Kimara.
Lengo la mradi huu ni kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 82 hadi 196 kwa siku ili kukidhi mahitaji hadi mwaka 2032. Mradi umekamilika na ulizinduliwa na Mh.Rais John Pombe Magufuli tarehe 21/06/2017. Ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilomita 69.569, jengo la Ofisi ya mradi Kibaha,ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita milioni 10 eneo la Kibamba, ukarabati wa matenki mawili yenye ujao wa lita milioni 8 kila moja yaliyopo Kimara Mwisho na kazi ya uunganishaji bomba jipya na la zamani eneo la Kimara Temboni umekamilika. Mtambo mpya kwa sasa unazalisha kiwango kilichokusudiwa cha mita za ujazo 196 kwa siku. Kukamilika kwa mradi huu umepunguza kero na uhaba wa maji katika miji ya Mlandizi na Kibaha pamoja na maeneo ya Kiluvya, Kibamba, Changanyikeni, Mbezi, Makabe, Msakuzi, Malamba Mawili, Matosa, Kimara, Kibangu, Makuburi, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Vingunguti, Airport, Ukonga, Kipawa na katikati ya Jiji la DSM.
Mradi wa visima virefu 20 Kimbiji na Mpera na Uchimbaji wa Visima vya Majaribio.
Lengo la mradi ni kuzalisha lita milioni 260 za maji kwa siku. Hadi sasa visima 19 kati ya 20 vimechimbwa na vipo katika hatua mbalimbali za uchimbaji. Utekelezaji wake umefikia asilimia 87.5. Visima vya maeneo ya Mpera vitahudumia wakazi wa maeneo ya Gongo la Mboto, Chanika, Luzando, Pugu, Mpera, Chamazi, Kitunda, Ukonga, Kinyerezi, na Uwanja wa Ndege; na visima vya maeneo ya Kimbiji vitahudumia wakazi wa maeneo ya Temeke, Kisarawe, Kibada, Kimbiji, Kigamboni, Tuangoma, Mkuranga, Kongowe, Mbagala, Kurasini, Mtoni, Tandika, Keko na Chang’ombe.
Mradi wa kupunguza upotevu wa maji (Non Revenue Water -NRW)
Mradi huu ni kwa ajili ya kupunguza uvujaji wa maji na maji yasiyolipiwa kutoka asilimia 36 ya sasa hadi asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.
Mradi wa Upanuzi wa Mfumo wa Kusambaza majisafi.
Lengo la mradi huu ni kuongeza mfumo wa usambazaji maji na kuunganisha wateja wote walioko katika maeneo yasiyo na mtandao na yale yatakayopata maji kutokana na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Chini na Ruvu Juu, pia maeneo yatakayopata maji ya visima vya Kimbiji na Mpera. Mradi huu umeanza kwa baadhi ya maeneo na uko katika awamu kuu mbili ambazo ni:-
Kazi hii inahusu miradi ya mabomba madogo na makubwa pamoja na kuunganisha wateja kwenye eneo kati ya Mbezi hadi Kiluvya na Tegeta hadi Bagamoyo. Jumla ya Km 511.6 za mabomba na matenki 5 yenye ujazo wa lita milioni 5 (moja) na lita milioni 6 (manne) yatajengwa. Ulazaji wa mabomba unaendelea katika maeneo ya Mbezi-Kiluvya (Kundi 2D) ambapo hadi sasa amelaza mabomba ya Km 177. Aidha anaendelea pia na ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji katika maeneo ya Changanyikeni, Wazo, Bunju, Bagamoyo, na Salasala. Kwa ujumla hadi kufikia Oktoba 2017 kazi imefika asilimia 53. Utekelezaji wa kazi umechelewa kutokana kuchelewa kukamilika usanifu na uagizaji wa mabomba na viungio vyake.
Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza kero na uhaba wa maji katika maeneo ya Mpiji, Bagamoyo, Bunju, Mabwepande, Boko, Mbweni, Tegeta, Ununio, Wazo, Salasala, Kinzudi, Matosa, Mbezi Juu, Goba, Changanyikeni, Makongo, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani.
Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia itatekeleza mradi wa ulazaji wa mabomba madogo ya kusambaza maji na kuunganisha wateja katika katika eneo la mradi kati ya Chuo Kikuu ikiwemo Changanyikeni, Makongo, Goba, Salasala, Wazo, Kinzudi, Bunju, Vikawe na Bagamoyo. Zabuni zilitangzwa mapema mwezi Mei 2017. Mradi huu utatekelezwa na DAWASCO.
Mradi huu utahusu ulazaji wa mabomba ya Km 2000 na utaunganisha wateja wapya 500,000. Ripoti ya mwisho pamoja na vitabu vya zabuni zilipelekwa DAWASCO, Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Benki ya Dunia wako kwenye mazungumuzo ya kutafuta fedha za ujenzi.
Lengo ni kuendeleza chanzo cha maji kutoka Mpera na kutandaza mabomba ya kusafirishia maji kwenda kwenye matenki ya kuhifadhi maji yatakayojengwa Gongo la Mboto, Chanika, Luzando na Pugu na baadaye mabomba madogo ya ugawaji katika makazi ya watu (Mpera, Chamazi, Gongo la Mboto, Chanika, Kitunda, Luzando, Pugu, Ukonga, Kinyerezi na Uwanja wa Ndege). Maoni au kibali kutoka Wizara ya Fedha yanasubiriwa.
Lengo ni kuendeleza chanzo cha maji kutoka Kimbiji na kutandaza mabomba ya kusafirishia maji kwenda kwenye matenki ya kuhifadhi maji yatakayojengwa Temeke na Kisarawe II (Kibada) na baadaye mabomba madogo ya ugawaji katika makazi ya watu (Temeke, Kisarawe II, Kibada, Kimbiji, Kigamboni, Tuangoma, Mkuranga, Kongowe, Mbagala, Kurasini, Mtoni, Tandika, Keko na Chang’ombe. Uchambuzi wa zabuni unaendelea.Utekelezaji wake utaanza mara tu baada ya kupata kibali cha fedha kutoka Benki ya Exim China
Mradi huu utahusu utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 100,000 wa Dar es Salaam, ambao hawajaunganishwa kwenye mtandao rasmi wa DAWASA. Ufumbuzi uliopendekezwa ni pamoja na hatua za ubia, ambayo inaweza kuwa kipimo cha muda mfupi cha kuunganishwa kwenye mtandao wa maji wa DAWASA kama hali hii inavyoongezeka katika maeneo kwa baadaye, ambapo mtandao wa maji ya bomba iliyopo haipatikani, mifumo ya ugavi wa maji ya mabomba madogo ya kujitegemea itakuwa huru kutekelezwa. Katika baadhi ya maeneo haya, ambapo mtandao wa mabomba iliyopo haujafikia, mifumo ya kujitegemea ya maji yenyewe imewekwa na inaendeshwa. Mradi huu, utahusisha mifumo ya maji ya bomba, chanzo cha maji, mfumo wa usambazaji wa jamii, vituo vya kuchotea maji katika jamii na / au ngazi ya kaya.Utekelezaji wa mradi huu utarekebisha, kupanua au ujenzi wa mifumo mipya, katika maeneo ambayo mtandao wa maji ya mabomba hautafika katika kipindi cha miaka 5-10. Aidha, mradi huu utaunganishwa kwenye mtandao wa mabaomba ya DAWASCO, mara tu upanuzi wa maeneo haya utakapochukua nafasi.
Mradi wa Upanuzi wa Mfumo wa Kusambaza Maji Maeneo ya kuanzia Mbezi hadi Kibaha na Changanyikeni hadi Bagamoyo.
Lengo la mradi huu ni kuongeza mfumo wa usambazaji maji kwenye maeneo yaliyopo kati ya Changanyikeni na Bagamoyo kutoka mitambo ya Ruvu Chini na kati ya Mbezi kwa Msuguri hadi Kibaha kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambapo hadi sasa ujenzi umefikia 15%. Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza kero na uhaba wa maji katika maeneo ya Changanyikeni, Salasala, Makongo, Wazo, Goba na Bunju, Mapinga, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya, Bagamoyo mjini na ukanda maalum wa EPZA.
Miradi ya Kuboresha na Kupanua Mfumo wa Uondoshaji Majitaka
Usanifa wa mradi wa majitaka Dar es salaam na uwasilishaji wa taarifa ya usanifu na nyaraka za zabuni umekamilika. Hatua inayofuata ni Usanifu wa kina (Detailed design) utakaofanywa na kila mkandarsai kwa mfumo wa Kusanifu, Kujenga na Kusimamia (Design, Build and Operate).
Mradi huu umegawanywa katika maeneo makuu matatu kulingana na jiografia ya Dar es Salaam:-
Itahusu ujenzi wa mfumo wa majitaka wenye mabomba yenye urefu wa kilomita 376 kuanzia Ubungo hadi Jangwani, Kinondoni na Mwananyamala, Msasani, Katikati ya jiji na Ilala ikiwa ni pamoja na kubadili mwelekeo wa bomba linalomwaga maji baharini na kuyapeleka kwenye mtambo wa Jangwani. Majitaka katika kundi hili yatasafishwa katika mtambo mpya utakaojengwa eneo la Jangwani. Mtambo huu utakuwa na uwezo wa kusafisha mita za ujazo 200,000 kwa siku. Hata hivyo mtambo huu utajengwa kwa awamu na awamu ya kwanza ni mtambo wenye uwezo wa mita za ujazo 25,000 kwa siku na mabomba kilomita 17.43 eneo la Magomeni.
Manispaa ya Ilala wamekabidhi eneo la ujenzi kwa DAWASA tarehe 22/9/2017 na eneo limejengwa uzio ili lisivamiwe.
Utaratibu wa manunuzi ya mshauri atakayefanya usanifu wa kina na kusimamia ujenzi ulianza Februari 2017 ambapo DAWASA iliwasilisha Exim Bank ya Korea rasimu ya mpango wa manunuzi (Procurement Plan) na nyaraka za zabuni ya kumtafuta mshauri (Request for Proposal) atakayefanya usanifu wa kina na kutayarisha nyaraka za zabuni za ujenzi. Tangazo la kukaribisha maombi (Invitation for Expression of Interest) ya washauri watakaofanya usanifu wa kina na kusimamia ujenzi lilitoka magazetini tarehe 27/3/2017 na tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ilikuwa tarehe 26/4/2017. Uchambuzi wa maombi umekamilika na taarifa iliwasilishwa Exim Bank ili kupata kibali cha kuendelea na hatua inayofuata (RFP). RFP imekamilishwa kwa kuingiza maoni ya Benki na kuirejesha tena Benki ili watoe kibali kugawa RFP kwa makampuni ya ushauri yaliyochaguliwa. Benki wameomba ufafanuzi kutoka Hazina kuhusu utaratibu mpya wa msamaha wa kodi (VAT). Majibu ya Hazina yanasubiriwa.
DANIDA wameonesha nia ya kushiriki kutekeleza mradi wa Majitaka maeneo ambayo hayajapata ufadhili kwa maeneo ambayo yatabaki baada ya mradi wa Korea ikiwemo Ilala, Ubungo, Sinza, Kinondoni, Mwananyamala, Oysterbay, Masaki na Msasani.Ujenzi wa mtambo wa kusafisha majitaka wenye ukubwa wa 50,000 -75,000m3/siku. Uamuzi wa DANIDA Unasubiriwa
.
Itahusu ujenzi wa mfumo wa mabomba ya majitaka upatao kilomita 90 katika maeneo ya Keko, Chang’ombe, Kurasini Temeke na Uwanja wa Taifa. Majitaka kutoka katika maeneo haya yatasafishwa katika mtambo mpya utakaojengwa maeneo ya Kurasini yalipo mabwawa ya kusafisha majitaka. Mtambo wa Kurasini utakuwa na uwezo wa kusafisha majitaka mmita za ujazo 11,000 kwa siku. Ulipaji wa fidia kwa wakazi wanaodai katika eneo lililopendekezwa unaendelea.
Itahusu ujenzi wa mfumo wa mabomba ya majitaka yenye urefu upatao kilomita 97 katika eneo la Mbezi Kawe, Mbezi Beach na Kilongawima. Majitaka katika kundi hili yatasafishwa katika mtambo mpya utakaojengwa maeneo ya Mbezi Beach, mtambo huu utakuwa na uwezo wa kusafisha majitaka mita za ujazo 16,000 kwa siku. Benki ya Dunia wanasubiri ukamilishaji wa taratibu za kupata eneo la kujenga mtambo Mbezi beach (Kilongawima).
Usanifu wa mradi huu unafanywa na Mtaalamu mshauri M/s Bureau for Industrial Cooperation (BICO) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa ya Usanifu imewasilishwa mwezi Septemba 2017. Mradi huu utahusisha ujenzi wa miradi midogo 50 ya kutibu Majitaka (DEWATs) katika Jiji la Dar es Salaam unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.Mradi huu unalenga uboreshaji wa huduma ya Majitaka na Usafi wa Mazingira.
Miradi ya visima vya dharura katika maeneo yasiyo na Mtandao
1.4.2 Mipango ya Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa” BRN” inayotekelezwa na Halmashauri za Manispaa.
Mkoa wa Dar es Salaam unatekeleza jumla ya miradi 41 ya visima vya maji katika Halmashauri za Manispaa ya Ilala, Kigamboni, Kinondoni, Temeke na Ubungo chini ya mpango wa BRN katika sekta ya Maji hususani Maji Vijijini ambayo ni mojawapo ya Sekta 6 zinazotekeleza Mpango wa BRN. Miradi yote iliyokuwa inatekelezwa chini ya Programu ya Maji (RWSP) katika Mkoa wa Dar es salaam iliingizwa katika mpango wa utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Mitaa iliyopewa kipaumbele katika kupata huduma ya maji kupitia Awamu ya Kwanza ya utekelezaji wa Programu chini ya Programu Ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini katika Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam vimeoneshwa kwenye Jedwali Na. 2.
Jedwali Na. 2: Mitaa iliyopewa Kipaumbele na Halmashauri katika kutekeleza
HALMASHAURI |
MITAA ILIYOPEWA KIPAUMBELE |
Ilala MC
|
Pugu Kajiungeni, Kipunguni B/ Mji mpya na Kivule/ Shule ya Msingi
|
Kigamboni MC
|
-
|
Kinondoni MC
|
Makongo Mbuyuni
|
Temeke MC
|
Toangoma/ Goroka, Mianzini, Mbagala/KizingaBughidad na Chalambe/Mashine ya Maji
|
Ubungo MC
|
Hondogo Kibwegere na Mpiji Magohe
|
1.4.3 Hali ya Utekelezaji wa Miradi hadi Septemba 2017.
Chini ya Mpango wa BRN, jumla ya Miradi ya Maji 41 ilikuwa imepangwa kutekelezwa. Hadi kufikia mwezi Septemba 2017 jumla ya miradi 17 ilipangwa kujengwa, miradi 6 ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji na miradi 11 ya Goroka, Kizinga Bughdadi, Mashine ya maji na Mianzini iliyopo katika Manispaa ya Temeke, Kibwegere, Mpijimagohe katika Manispaa ya Ubungo, Makongo Mbuyuni na Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni pamoja na Pugu Kajiungeni, Kipunguni B na Kivule katika Manispaa ya Ilala imekamilika na imeshaanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi kama ambavyo inaonekana katika Jedwali Na. 3. Aidha, katika kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelevu, miradi yote inaendeshwa na wananchi wenyewe kupitia Vyombo vya Watumiaji Maji/Vikundi vinavyoundwa kisheria.
Jedwali Na. 3: Miradi iliyopangwa kutekelezwa na inayotekelezwa
Maelezo ya Miradi ya BRN iliyopendekezwa
|
Miradi iliyopangwa kutekelezwa hadi kufikia Novemba, 2017/2018
|
|||||
Ilala MC
|
Kigamboni MC |
Kinondoni MC |
Temeke MC |
Ubungo MC |
Jumla ya Miradi
|
|
Miradi ya Maji ya Vijiji 10 (WSDP)
|
03 |
03 |
01 |
08 |
02 |
17 |
Miradi ya Ukarabati na/au upanuzi
|
00 |
00 |
01 |
00 |
00 |
01 |
Miradi ya Quickwin
|
00 |
00 |
00 |
00 |
00 |
00 |
Miradi ya Kitaifa
|
00 |
00 |
00 |
00 |
00 |
00 |
JUMLA
|
03 |
03 |
02 |
08 |
02 |
18 |
Aidha, Maelezo ya kina ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu katika miradi ya maji ya Vijiji 10 vilivyoainishwa na Halmashauri husika kulingana na fedha iliyotengwa umefanyika kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 4:
Jedwali Na. 4: Hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Miradi ya Maji hadi mwezi Septemba 2017
Halmashauri
|
Jinala Mradi/Mtaa unaotekelezwa
|
Hatua iliyofikiwa ya utekelezaji
|
Ilala MC
|
Pugu Kajiungeni, Kipunguni B/ Mji mpya na Kivule/ Shule ya Msingi
|
Mradi wa Pugu Kajiungeni unatoa huduma kwa Wananchi
Mradi ya Kipunguni B umekamilika na unatoa huduma kwa Wananchi Mradi wa Kivule ipo katika hatua ya majaribio |
Kigamboni MC
|
Chambewa, Kibene na Malimbika
|
Mradi wa Chambewa umefikia hatua ya 60%
Miradi ya Kibene na Malimbika imefikia hatua ya 25% |
Kinondoni MC
|
Makongo Mbuyuni na Mabwepande
|
Miradi imekamilika na inatoa huduma ya maji kwa Wananchi
|
Temeke MC
|
Toangoma/ Goroka, Mianzini, Mbagala/KizingaBughidad, Chalambe/Mashine ya Maji, Mbuyuni/Azimio, Mamboleo B/ Sandali na Mabatini/ Tandika
|
Miradi ya Goroka, Mianzini, Kizinga Bughidad na Mashine ya Maji imekamilika na inatoa
huduma ya maji kwa Wananchi Miradi ya Azimio, Mamboleo B na Tandika imefikia hatua ya 50% na utekelezaji wa miundombinu ya maji unaendelea |
Ubungo MC
|
Hondogo Kibwegere na Mpiji Magohe
|
Miradi imekamilika na inatoa huduma ya maji kwa Wananchi
|
1.4.4 Miradi Mingine inayotekelezwa kwenye Halmashauri
Kupitia bajeti za Halmashauri (Own Source, UNICEF, LGCGD, BTC, WATER AID, Africa Relief, na mfuko wa Jimbo) Halmashauri zote tano zinaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika maeneo yao kama ifuatavyo:-
Manispaa ya Ilala
Katika Manispaa ya Ilala, jumla ya Miradi 7 katika maeneo ya Pugu Bangulo, Kinyerezi, Bonyokwa, Pugu Kinyamwezi, Pugu Kichangani, Ulongoni A pamoja na Lada ujenzi wake umekamilika na imeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Miradi 5 katika maeneo ya Lubakaya, Lukooni, Mkera, Segerea na upanuzi wa mradi wa usambazaji wa maji katika maeneo ya Kinyamwezi, Mustafa naViwege ujenzi wake unaendelea na upo katika hatua nzuri.
Manispaa ya Kigamboni
Manispaa ya Kigamboni kuna jumla ya Miradi 2, mradi wa Mwasonga-Kisarawe II ujenzi wake umekamilika na umeanza kutoa huduma ya maji na Minondo Somangila ujenzi unaendelea inasubiriwa kupitisha nguzo za umeme wa TANESCO kwa ajili ya ukamilishaji.
Manispaa ya Kinondoni
Jumla ya Miradi 2 ya Makongo Juu na Kigogo Buyuni imekamilika na inatoa huduma ya maji.
Mradi wa maji wa Mivumoni ukarabati wake unaendelea.
Mradi wa maji Shule ya Msingi Changanyikeni ujenzi wake umefikia 75% na kazi inaendelea.
Manispaa ya Temeke
Manispaa ya Temeke, jumla ya Miradi 3 ya Kurasini-Mvinjeni, Buza na Makuka ujenzi wake umekamilika na imeanza kutoa huduma ya maji.
Mradi wa Maji unaohusisha uboreshaji wa huduma ya maji katika kata tatu maeneo ya Kibondemaji unaotekelezwa kwa msaada wa Shirika la Water Aid/PDF ujenzi wake umekamilika na umeanza kutoa huduma kwa jamii.Mradi unahudumia Wananchi 13,520.
Mradi wa Maji wa Mkondogwa unaendelea na ujenzi wake upo hatua za mwisho za ukamilishaji.
Ujenzi wa mfumo wa kutibu Majitaka (DEWATs) katika eneo la Toangoma unaotekelezwa kwa msaada wa wa Shirika la Water Aid/PDF, ujenzi wa mradi unaendelea ambapo hadi sasa umefikia 90%, kazi zilizobaki ni kukamilisha mifuniko ya chemba, ujenzi wa fensi na kusawazisha eneo.
Manispaa ya Ubungo
Jumla ya Miradi 3 ya Makurumla mnara wa Voda, Makurumula sisi kwa sisi na Nzasa A imekamilika na inatoa huduma ya maji.
Ujenzi wa mfumo wa kutibu Majitaka (DEWATs) katika eneo la Mburahati/ Barafu, uandaaji wa eneo kwa ajili ya ujenzi umeanza.
2.0 MAFANIKIO
Kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa Ruvu Chini ambao umeongeza upatikanaji wa Maji kutoka Lita Milioni 182 na kufikia lita milioni 270. Mradi umekamilika Mwezi Machi, 2016 na unatoa huduma ya maji kwa Wananchi.
Kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa Ruvu Juu ambao umeongeza upatikanaji wa Maji kutoka Lita Milioni 82 na kufikia lita milioni 196. Mradi umekamilika Mwezi Aprili, 2017 na unatoa huduma ya maji kwa Wananchi.
Upotevu wa Maji umepungua (Non Revenue Water) kutoka 45% hadi 36%
Kukamilika Visima 19 kati Visima 20 vya Kimbiji na Mpera ambavyo vitaongeza upatikanaji wa Maji kwa Lita Milioni 260 ifikapo mwaka 2019/20
Kukamilika kwa miradi ya Visima 15 vya ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji (BTC) ambayo inahudumia zaidi watu 250,000.
Kukamilika kwa miradi ya visima 8 vya mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (BRN) ambayo inahudumia zaidi watu 120,000.
Matarajio ya Mkoa ni kuwapatia watu huduma ya Majisafi kwa asilimia 95 ya wakazi wote na uondoshaji wa Majitaka kwa asilimia 30 ifikapo mwezi Desemba 2025.
Changamoto kubwa katika utoaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam ni kasi ndogo ya uwekezaji ukilinganishwa na kasi kubwa ya ongezeko la watu. Ongezeko kubwa la watu Jijini hasa kuanzia miaka ya 1980 kwa kiasi kikubwa limechangia katika kuongeza mahitaji ya maji. Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wanaendelea na juhudi za kutafuta fedha ili kuendeleza miradi ya maji kwa lengo la kukabiliana na mahitaji ya sasa na baadaye. Changamoto zingine ni pamoja na:-
S/No
|
CHANGAMOTO
|
MIKAKATI
|
1
|
Uhaba wa vyanzo vya maji na kasi ya ongezeko la mahitaji (wakazi)
|
Upanuzi wa mitambo ya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini, uchimbaji wa visima virefu vya maji Kimbiji/Mpera, ujenziwa Bwawa la Kidunda
|
2
|
Ukame, uvamizi na uchafuzi wa vyanzo
|
Kushirikiana na Wizara (Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu) katika kulinda vyanzo husika
|
3
|
Upatikanaji wa maeneo ya kujenga miundombinu
|
Kuendelea kuwasiliana na Ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika kupata maeneo ya kujenga miundombinu na pia kutumia way leave zilizopo kwa kukabiliana na taasisi husika
|
4
|
Uvamizi na ujenzi holela katika maeneo ya miundombinu.
|
Ushirikishwaji wa Jiji, Manispaa na Wizara ya Ardhi katika Upangaji wa Miji.
|
5
|
Wizi wa maji, uharibifu na wizi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka,
unachangia kiwango kikubwa cha maji yasiyolipiwa (zaidi ya asilimia 45) pamoja na uchafuzi wa maji. |
Kushirikiana na wananchi, vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda miundombinu na kuzuia wizi wa maji na uharibifu wa miundombinu na uchafuzi wa maji.
|
6
|
Kiwango kikubwa cha maji yasiyolipiwa
|
Kuweka dira za maji kwa wateja, kuanzisha utumiaji wa “data loggers“ katika usomaji wa dira za wateja na upanuzi wa mfumo wa usambazaji majisafi
|
7
|
Gharama kubwa za uendeshaji ikilinganishwa
na mapato |
Maombi ya kuongeza gharama za ankara za maji yamewasilishwa EWURA
|
8
|
Mfumo wa kuondoa majitaka haujafika maeneo mengi ya Jiji
|
Usanifu wa kuongeza mfumo wa uondoshaji majitaka umekamilika, utekelezaji wake unasubiri upatikanaji wa fedha utahusisha kampuni binafsi kupata fedha zaidi za kutekeleza miradi hii, sambamba na upatikanaji wa fedha kutoka serikali kuu
|
9
|
Ufinyu wa bajeti ya kutekeleza miradi mipya ya maendeleo na Upatikanaji wa fedha za miradi kwa wakati
|
Serikali inaendelea na utafutaji fedha kutoka kwa Wadau wa Maendeleo na kutenga kwenye bajeti kwa ajili ya Utekelezaji miradi mikubwa.
|
4.0. Mwisho
Tunatoa wito kwa Wadau na watumiaji wa huduma ya maji Mkoa wa DSM kulipia Ankara za maji kwa wakati, kuepuka wizi wa maji na uharibifu wa miundombinu ya maji, kulinda miundombinu iliyopo nainayojengwa ili huduma ya maji iwe endelevu. Aidha, ulinzi shirikishi wa vyanzo vya maji ni budi upewe kipaumbele katika ngazi zote, pia wananchi kutoa taarifaya ya uvujaji wa maji ili kuweza kupunguza upotevu wa maji.
"MAJI NI UHAI NA USAFI WA MAZINGIRA NI UTU"
Kiambatisho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa