Mgombea Urais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya mikutano ya kampeni jijini Dar es salaam kuanzia oktoba 21 hadi oktoba 23 mwaka huu ikiwa ni katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais Wabingu na Madiwani unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025
Akizungumzia ujio wa mgombea huyo ambaye ni Rais wa Jamhuri ua muungano wa Tanzania, RC Chalamila amesema mgombea huyo anatarajia kufanya kampeni kwenye viwanja vya Leaders Club,viwanja vya TANESCO- Temeke na viwanja vya kinyerezi jijini humo hivyo amewataka wananchi kujitokeza ili kisikiliza sera za mgombea huyo
Aidha Chalamila amewahakikishia wananchi wa Mkoa huo kuwa ni salama na utaendelea kuwa salama katika kipindi chote cha kampeni,wakati wa uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi, hivyo amewataka wananchi kushiriki shugjuli zote za uchaguzi na kujitoleza kupiga kura Oktoba 29 bila kuhofia vitisho vya aina yoyote.
Hata hivyo RC Chalamila amezungumzia changamoto za upungufu wa maji kwenye mkoa huo ambapo amewatoa shaka wananchi kuwa hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa sasa changamoto hiyo inakwenda kupata suluhisho la kudumu ambapo tayari zimenunuliwa mashine mpya za kusukuma maji pia amezungumzia bwawa la kidunda ambalo litamaliza kabisa changamoto ya maji katika Mkoa huo
Sanjari na hilo RC Chalamila amezungumzia suala la umeme kwenye mkoa huo ambapo amesema upatikanaji wa umeme umeimarika na kwamba Serikali inaendelea na mchalato wa kukabiliana na changamoto ya mafuriko kwa kujenga madaraja ya Jangwani, Kigogo na Mkwajuni pamoka na madaraja ya geti jeusi na nguva yaliopo kigamboni
Hata hivyo RC Chalamila amezungumzia kuimarika kwa usafiri wa mwendokasi jijini humo ambao kwa sasa Serikali imeamumua kufanya kazi na sekta binafsi ambapo amepiga marufuku kwa daladala bajaji na bodaboda kupita kwenye njia ya mwendolasi ili kiruhusu usafiri huo kutimiza lengo lililokisudiwa la kuwa usafiri wa Haraka
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa