
-Hundi ya mikopo ya asilimia 10 kundi la Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Januari 27, 2026 amekabidhi Hundi ya thamani ya Shilingi Bilioni 7.5 (7,517,146,645) ikiwa ni fedha ya mikopo inayotokana na 10% ya Mapato ya ndani ya Manispaa inayokwenda kutolewa kwa kundi la Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo RC Chalamila amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha wanaitumia vizuri kama nyenzo bora ya kujikwamua kiuchumi ili iwanufaishe katika maisha yao na kuwawezesha kurudisha mikopo hiyo kwa wakati.
"Mkaendelee kujipanga vizuri kwenye mikopo hii ili mkawe matajiri muongeze kipato chenu, pia hakikisheni mikopo hii irejeshwe kwa wakati", alisema RC Chalamila.
Vikundi 4 vya Wanawake vimepata Bilioni 3, Vikundi 2 vya walemavu vimepata Bilioni 1.5, huku Vikundi 4 vya Vijana navyo vikipatiwa Bilioni 3.
Aidha, Mhe. Chalamila amewahimiza Wananchi kuendelea kudumisha Amani na utulivu wa nchi ili kutengeneza mustakabali mzuri wa Taifa akimtaka Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda kuhakikisha anashugulikia Migogoro mbalimbali ya Wananchi ikiwemo Migogoro ya Ardhi, Ndoa na Mirathi ili Wananchi ambapo amewasii waendele kuishi kwa amani, upendo na utulivu

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa