
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Feb 16,2026 amezindua rasmi utoaji wa huduma bure za kisheria kwa wananchi katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini humo.
RC Chalamila akizindua huduma hiyo amesema kuwepo kwa huduma bure ya kisheria kutasaidia kupunguza mashauri au migogoro dhidi ya Serikali, malalamiko ya kisheria kutoka kwa wananchi, vitendo vya uonevu vinavyovunja sheria na taratibu pia kwa kuwa kuna kamati za mashauri ya kisheria nazo zitatoa elimu ya sheria kwa umma katika kushughulikia changamoto mbalimbali katika maeneo yao.
Aidha RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuandaa klinik hiyo ambayo inatimu ya Mawakili wabobevu ambao watakuwa wanatoa huduma za kisheria bila malipo kwa wananchi wote watakaohudhuria katika viwanja hivyo kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa jirani.


"Migogoro mingi na mikubwa katika Mkoa wa Dar es Salaam huchangiwa na tamaa ya mali ni muhimu kuielimisha jamii kufanya kazi kwa bidii na kujielekeza kumiliki mali na sio urithi wa mali" Alisisitiza RC Chalamila
Ifahamike kuwa uzinduzi wa kamati za ushauri wa kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam umefanyika leo feb 16, 2026 na kufuatiwa na kliniki ya Sheria bila malipo kwa wananchi kuanzia tarehe 16 hadi 22 Feb 2026 katika viwanja hivyo vya Mnazi mmoja

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa