• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Miundombinu

Seksheni hii ina lengo la kutoa huduma za kitaalamu zinazohitajika kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza Miundombinu na inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Majukumu ya Seksheni ya Miundombinu:

  • Kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Viwango katika nyanja za Barabara, Majengo, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
  • Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika nyanja za Barabara, Majengo, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
  • Kuwasiliana/kuwa daraja kuunganisha baina ya Mamlaka zinazohusika kwenye Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya masuala ya Ujenzi
  • Kushauri juu ya Masuala ya barabara, Ujenzi, Viwanja na uboreshaji mifumo
  • Kusimamia na kushauri juu ya kazi za Ujenzi zinazotekelezwa ndani ya Mkoa
  • Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kutwaa ardhi kwa ajili ya matumizi ya Serikali Kuu
  • Kuandaa ramani kwa ajili ya mipangomiji
  • Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya Tathimini ya Athari za Kimazingira


BARABARA

Mtandao wa barabara za Mkoa wa Dar es Salaam una urefu wa km 2094.4 ambapo kati ya hizo TANROADS inasimamia na kuhudumia barabara zenye urefu wa km 494.3 na zilizobaki km 1600.1 ziko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa za Ilala (km 429), Kinondoni (km 692.7) na Temeke (km 478.4). Halmashauri ya Jiji haina barabara inayoisimamia.
 
 Mtandao wa barabara umegawanyika katika makundi yafuatayo:
• Barabara kuu (Trunk roads):
Barabara kuu zote ambazo ni barabara za Morogoro, Kilwa, New Bagamoyo, Nyerere/Pugu,na Mandela/Sam Nujoma zina urefu wa km 126.2
 
•  Barabara za Mkoa (Regional Roads):
Barabara za Mkoa zote zinazosimamiwa na TANROADS zina urefu wa km 368.3
 
Barabara zilizoko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa
•  Barabara za Halmashauri (District & Feeder roads)
Barabara za Halmashauri ni zile zenye urefu km 1600.1 zilizoko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa za Ilala (km 429), Kinondoni (km 692.7) na Temeke (km 478.4).
 
 Miradi ya Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara Mkoani

 
Kwa kushirikiana na Shirika la Msaada la JAPAN (JICA) mpango kabambe wa usafiri na usafirishaji umeandaliwa. Mpango huu utatumika katika uendelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu na aina mbalimbali za usafiri na uchukuzi hadi mwaka 2030.


Jedwali la Mtandao na Aina za Barabara Mkoani Dar es Salaam

Msimamizi

Urefu wa Barabara(km)
Aina ya barabara(km)
Lami
Changarawe
Udongo
Tanroads

494.3

211.4

282.9

Ilala

429

132

80

217

Kinondoni

692.7

114.7

315.25

262.752

Temeke

478.4

67

411.11

Jumla

2094.4

525.1

1569.3


ARDHI

Umiliki wa Ardhi

Baada ya miaka 52 ya Uhuru maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam yalikaliwa na wazawa ambapo maeneo hayo yapo kati ya eneo la kati la biashara (CBD) Kariakoo, Ilala, Magomeni yamekuwa yakiuzwa kwa watu wenye uwezo wa maendelezo ya majengo ya ghorofa. Utoaji wa miliki za Ardhi umekuwa ukitolewa kwa kasi na kwa kutumia TEKNOHAMA ikilinganishwa na miaka kabla ya Uhuru hadi miaka ya 1999.
Baada ya Halmashauri ya Jiji kuvunjwa na Tume ya Jiji kuwepo na kisha baadaye Halmashauri tatu za Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke kuundwa mwaka 2000 idadi ya Hati miliki nyingi zimetolewa.
Hati miliki za viwanja zimekuwa zikitolewa kwa ushirikiano na Wizara ya Ardhi ambayo imeunganishwa na Halmashauri kwa njia ya Mtandao. Vile vile, kodi za Ardhi zimekuwa zikikusanywa kwa utaratibu huo.
Baada ya miaka 52 ya Uhuru sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 namba 4 na 5 Ardhi imekuwa ikitumika na thamani katika miaka 52 ya Uhuru ni wazi kuwa thamani ya utwaaji Ardhi imekuwa ni ghali ikilinganishwa na wakati kabla ya Uhuru.

Uendelezaji upya wa eneo la Magomeni Quarter

Uzoefu wa Miaka 52 ya Uhuru ni kuwa viwanja vimeanza kuuzwa kutokana na upandaji wa gharama za utwaaji, upimaji na uandaaji miliki ya viwanja baada ya sheria namba 4 ya Ardhi ya mwaka 1999 kuanza kutekelezwa. Uuzaji viwanja ulianza rasmi kwenye Mradi wa Upimaji viwanja elfu ishirini (20,000) chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Maeneo ya Viwanja vya masafa ya chini (Low Density Plot) yalijulikana kama Uzunguni, masafa ya kati yakiwa Uhindini na masafa ya juu (High Density) kwa wananchi wa kawaida. Miliki ya viwanja vya masafa ya chini Low Density ni miaka 99, kwa viwanja vya masafa ya kati miaka 66 na miaka kwa viwanja vya masafa ya juu kuwa miaka 33. Offer au Hati za muda zilitolewa na baadaye hati za kudumu.
Mwaka 2005 zilitolewa Hati miliki 7,125 Wakati 2013 zilitolewa 19,111, kwa ujumla katika kipindi hiki hadi Desemba, 2013 zimetolewa jumla ya hati miliki 26,236.

 Aidha, mwaka 2005 leseni za makazi zilianza kutolewa hadi Desemba, 2013 zimetolewa jumla ya leseni za makazi 51,049 katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mapendekezo ua Uendelezaji wa wa eneo la Mchikichini

Mipangomiji na Udhibiti wa Matumizi Bora ya Ardhi

Mamlaka ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mpango wa matumizi ya Ardhi hata kabla ya Uhuru ambapo maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali yalitengwa. Matumizi hayo kulingana na mpango kabambe yalitengwa kwa kuzingatia matabaka ya watu na uwezo wa kifedha.

Aidha, kuongezeka kwa uhitaji wa viwanja na kupungua kwa uwezo wa Mamlaka za Jiji kupewa viwanja vilivyopimwa yalisababisha makazi holela kuongezeka.

Baada ya miaka 52 ya Uhuru Mamlaka za Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam zimekuwa na mikakati mbalimbali ya kuandaa matumizi ya Ardhi, kuendeleza upya maeneo ya kati, kudhibiti ukuaji holela wa makazi, kurasimisha makazi holela na kuandaa mpango kabambe wa Jiji. Mpango wa uendelezaji upya na maeneo ya Kariakoo, Upanga, Msasani, Temeke, Ilala, Magomeni, Msasani na Osterbay umeandaliwa na kuanza kutekelezwa.

Ukuaji wa Jiji umefanyika kwa kila upande ukielekea kwenye njia kuu za kuingia katikati ya Jiji kwenye Bandari. Ukuaji huo zaidi ya asilimia 75 ni makazi holela na asilimia 25 ni maeneo yaliyopangwa kimipangomiji na kupimwa. Aidha Serikali imekuwa na juhudi mbalimbali za kudhibiti uendelezaji holela wa Jijini kama vile uanzishaji wa Mamlaka za Uendelezaji Mji wa Kigamboni inayoitwa Kigamboni Development Agency (KDA). Mamlaka hii imepewa mamlaka ya kusimamia na kuratibu uendelezaji upya wa eneo la Kigamboni kuwa Jiji la Kisasa na lenye hadhi ya Kimataifa.

Kulingana na mpango kabambe wa Jiji la Dar es Salaam ulioko kwenye hatua za maandalizi, Mkoa wa Dar es Salaam una ardhi yenye eneo la hekari 161,796,384 ambazo ni sawa na kilometa za mraba 1,617.96.

Bonyeza hapa kupata takwimu za Matumizi ya ardhi katika Jiji la Dar es Salaam

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Masoko Mapya Yatakayojengwa Washirikishwe Machinga na Viongozi wa Soko

    March 11, 2023
  • RC Makalla Aeleza Kishindo Cha Rais Dkt Samia Suluhu Miaka 2 DSM

    March 10, 2023
  • RC Makalla Atimiza ahadi ya Kuwapeleka Viongozi wa Machinga Taifa Kigali Rwanda

    March 10, 2023
  • RC Makalla Hakuna Fremu Soko la Kariakoo Zilizogawiwa Epukeni Matapeli

    March 26, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akikagua Maendeleo ya Ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa