Wilaya ya Kigamboni iliundwa kutokana na wilaya mama ya Temeke kupitia Tangazo la Serikali Na. 462 la mwaka 2015 kuhusu mgawanyo wa Wilaya. Wilaya ya Kigamboni ina ukubwa wa kilomita za mraba 416. Aidha, Wilaya ya Kigamboni inapakana na Bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki, Wilaya ya Mkuranga upande wa kusini, kaskazini inapakana na Bahari ya Hindi na upande wa magharibi ipo Manispaa ya Temeke
Kufuatia Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Wilaya ya Kigamboni ilikuwa na jumla ya watu 162,932 na kaya 40,133. Kati ya hao wanaume walikuwa 81,199 na wanawake walikuwa 81,733. Wilaya ya Kigamboni ina ongezeko la wakazi linalofikia asilimia 5.6 kwa mwaka hivyo hadi kufikia mwaka huu 2017, Wilaya ya Kigamboni inakisiwa kuwa na watu wapatoa 205,966 na Kaya 48,043. Kati yao wanaume ni 102,645 na wanawake ni 103,321.
Wilaya ya Kigamboni ina Tarafa 1, Kata 9 na Mitaa 67. Aidha, Wilaya ya Kigamboni ina Halmashauri 1 na Jimbo 1 la uchaguzi na inaundwa na Baraza la Madiwani lenye jumla ya wajumbe 15. Kati ya hao, madiwani tisa (9) ni wa kuchaguliwa na wanne (4) ni wa viti maalum. Aidha, wabunge wapo wawili (2) ambapo mmoja (1) ni wa jimbo na mmoja (1) ni wa viti maalum.
Kujua zaidi kuhusu Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, bofya hapa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa