
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewatangazia wakazi wa Mkoa huo hususani vijana kushiriki Tamasha la IST Festival linalotarajia kufanyika februari 14 mwaka huu kwenye viwanja vya Coco beach ikiwa ni katika kuunganisha wananchi na kuimarisha umoja,upendo na mshikamano baina ya yao.
Akizungumza katika viwanja vya Coco beach na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema anatambua kuwa hivi karibuni wananchi wametoka kwenye uchaguzi na wameingia mwaka mpya 2026 hivyo kupitia tamasha hilo itasaidia kuwaunganisha wananchi kuwa pamoja, kusherekea, pia kupeana fursa mbalimbali pamoja na zawadi ikiwemo magari aina ya IST kwa watakaoshiriki vyema.

Aidha RC Chalamila amesema kupitia Tamasha hilo wananchi watapata fursa ya kupima na kujua afya zao hususani kwenye changamoto za maradhi ya moyo ambapo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete inatarajia kushiriki kwa kutoa huduma za upimaji afya.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Nurdeen Bilali Jina maarufu kama Sheta amesema katika tukio hilo pia kutakua nyama choma ambayo watu watakula bila malipo hivyo wananchi wakazi wa jiji la Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi.
Ifahamike kuwa Kaulimbiu ya IST festival kwa mwaka 2026 inasema "Vimba na gari yako"

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa