• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Afika 'Site' Block D, Kunduchi Kutatua Mgogoro wa Nyumba ya Mama Mjane

Posted on: January 7th, 2026

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila mapema leo amefika eneo la mgogoro wa nyumba ya Mama mjane Block D Kunduchi Wilaya ya Kinondoni ambapo ameagiza kuundwa kamati maalumu chini ya ofisi yake huku pia akimueleleza mkuu wa wilaya ya kinondoni Mhe Saad Mtambule kuunda kamati nyingime ili kamati hizo ziweze kushughulikia kwa haraka mgogoro huo na haki ipatikane kwa wakati.

Mgogoro huo unahusisha nyumba pamoja na viwanja namba 38,39 na 40 blok D vilivyoko kunduchi beach Kinondoni, ukimhusisha Happiness Mwambingu ambae ni mjane wa marehemu Dkt Benard Mwambingu na Fots Mwambingu ambae ni mdogo wa marehemu alieamua kubadilisha hati ili kujimilikisha nyumba na viwanja vya aliekuwa kaka yake

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo na kusikiliza namna mgogoro huo ulivyo, pamoja na uamuzi wa kuunda kamati hizo mbili RC Chalamila ameliamuru Jeshi la polisi kumkamata Lidia Benard na Joel Mwambingu ambao walifanya udanganyifu ili kujimilikisha eneo hilo na hatimaye likauzwa ambapo Lidia Benard alijifanya ni mke wa marehemu huku Joel akijifanya ni Mtoto wa Marehemu.

Aidha kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amesema kwa kuwa kumekuwa na sintofahami nyingi kwenye viwanja na nyumba hiyo hadi kuuzwa na kwamba mjane huyo alipaswa kuondoka kwenye nyuma hiyo ameelekeza mjane huyo kuendelea kuishi hapo hadi pale watakapojiridhisha juu ya mmiliki halali

Sanjali na hilo Mjane wa marehemu Bi Happiness na Mwanasheria wa kamishna wa ardhi Adelifrida Lekule wameeleza hali halisi ya mgogoro huo ulivyo hadi kufikia hapo ulipo ambapo nyumba hiyo tayari imeuzwa na mjane huyo kutakiwa kuondoka kwenye nyumba hiyo.

Mwisho moja ya mambo yanayoleta utata ni kijana Joel kuwa yeye ni mmiliki wa nyumba na viwanja hivyo tokea miaka ya 1980 wakati yeye mwenyewe amezaliwa mwaka 1996

Matangazo

  • MWENENDO WA BEI WIKI YA 29 DISEMBA - 02JANUARI 2026 MKOA WA DSM January 05, 2026
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • MWENENDO WA BEI WIKI YA 1-5 DESEMBA 2025 December 01, 2025
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Afika 'Site' Block D, Kunduchi Kutatua Mgogoro wa Nyumba ya Mama Mjane

    January 07, 2026
  • Naibu Waziri wa Nchi OWM-TAMISEMI Mhe Kwagilwa Ahitimisha Ziara ya Kikazi Dar

    January 03, 2026
  • RC Chalamila " Tuendelee Kudumisha Amani Tunaposherekea Sikukuu ya Mwaka Mpya 2026"

    December 31, 2025
  • Dkt Mwigulu Nchemba Aunga Mkono Ujenzi wa Kituo cha Daladala Bunju B

    December 29, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa