
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi anatarajia kuzindua rasmi jengo la wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julias Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2026
Akizungumza Jijini Dar es salaam kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila mbele ya waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge amesema jengo hilo lililojengwa kwa fedha za Serikali katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Terminal 1 limekamilika kwa asilimia miamoja na kwamba sasa lipo tayari kuzinduliwa rasmi hapo kesho
RC Kunenge amesema jengo hilo litakua kwa ajili ya viongozi wa kitaifa,wakuu wa nchi mbalimbali wanaotembelea nchini Tanzania pamoja na wageni mashuhuri hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uzinduzi huo ambao utahudhuriwa ni viongozi mbalimbali.
Aidha Kunenge amesema uwanja huo ni moja ya vichocheo vya ukuaji wa uchumi kwa nchi ya Tanzania na kwamba wakati wa ujenzi wa jengo hilo maalumu vijana wengi hapa nchini walipata ajira hata hivyo kwa kuwa limejengwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, jengo hilo litaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi katika Mkoa na Taifa kwa Ujumla

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa