
-Asema Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Februari 3,2026 katika Mkoa wa Dar es Salaam
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa zana endelevu za kilimo Afrika yaani "Africa Sustainable Agricultural Mechanization" utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia februari 3 hadi 6, 2026 utakaokwenda sambamba na uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa zana za kilimo, awamu ya pili ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba anatarajia kuwa mgeni rasmi
Akizungumzia mkutano huo mbele ya waandishi wa jijini Dar es salaam RC Chalamila amesema mkutamo huo unafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya kilimo nchini Tanzania na shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa FAO ambao utatoa fursa ya kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano na kuharakisha juhudi za matumizi ya zana za kilimo kwa ajili ya mageuzi endelevu ya kilimo nchini na Afrika kwa ujumla
Aidha RC Chalamila ameongeza kuwa kupitia mkutano huo Waziri mkuu Dkt Mwigulu Nchemba anatarajia kuzindua mkakati wa Taifa wa zana za kilimo awamu ya pili ambao utakuwa ndiyo muongozo mkuu wa kuongeza tija nchini kupitia tekinolojia za kisasa za kilimo, mkutano ambao utahudhuriwa na Mawaziri wa kilimo kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wadau wa kilimo ikiwa ni miongoni mwa juhudi za Rais Dkt Samia kuimarisha kilimo kwa masilahi mapana ya Umma.

Kwa upande wa Mwakilishi mkazi wa shirika la kimataifa la chakula na kilimo FAO Charles Tulai amesema mkutano huo ni muhimu ili kuwezesha nchi za Afrika kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi na ongezeko la watu ambapo Tanzania imetajwa kuwa ni sehemu bora ya kufanyia mkutano huo huku vijana wakitajwa kama nguvu kazi muhimu kwenye kilimo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa