
-Atoa pesa tasilimu kwa ajili ya michezo na ahadi ya milioni 5 kwa shule ya msingi Goroka "A"
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila mapema leo Januari 27, 2027 ameongoza zoezi la upandaji miti na kukata Keki akiwa na uongozi wa Wilaya ya Temeke, pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Goroka 'A' iliyopo Kata ya Toangoma ikiwa ni Ishara ya Kusherehekea Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Daktari Samia Suluhu Hassan, tukio linalobeba ujumbe wa "Mazingira ni Utu na Maendeleo Endelevu".

RC Chalamila mara baada ya kukamilisha zoezi la Upandaji miti lililofanyika shuleni hapo ametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi na walimu pia ameahidi kutoa Shilingi Milioni Tano kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Goroka "A" ili kusaidia Utengenazaji wa Viti vya kukalia Walimu wa Shule hiyo.
"Mmefanya kazi kubwa sana kwa maendeleo yetu, Wiki ijayo nakuingizia milioni tano ya kutengeneza Viti vya kukalia Walimu", alisema RC Chalamila .
Vilevile Mkuu wa Mkoa amewashukuru Watumishi na Viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Temeke kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuleta Maendeleo kwenye Sekta mbalimbali katika wilaya hii.
Aidha RC Chalamila amekabidhi Shilingi laki tano kwa Shule hiyo ili kusaidia kuandaa Bonaza la michezo kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mwisho RC Chalamila amesistiza dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Daktari Samia Suluhu Hassani ni kukuza utalii katika kulinda mazingira na ukuzaji uchumi huku ikiweka msingi imara na urithi kwa vizazi vijavyo

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa