• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Afya na Ustawi wa Jamii

Seksheni hii lengo lake ni kuwezesha utoaji wa huduma bora za Afya za kinga, matibabu na maendeleo ya huduma za Afya na Ustawi wa Jamii katika Mkoa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa, ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Idara ndogo ndogo ndani ya Afya

  1. Elimu ya Afya
  2. Huduma za Tiba (Magonjwa ya ndani, Watoto, wajawazito, Upasuaji na Mifupa, Huduma za mionzi, Maabara na Mortuary)
  3. Huduma za Kinga (Huduma za Afya ya mama na mtoto na Huduma za kuzuia magonjwa ya kuambukiza)
  4. Utengemao (Rehabilitation)
  5. Ustawi wa Jamii
  6. Afya ya Mazingira


Majukumu ya Seksheni ya Afya na Ustawi wa Jamii:

  • Kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa wa sera za Afya katika Mkoa
  • Kuratibu masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Mkoa
  • Kusimamia utoaji sahihi wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali/vituo vya Umma na sekta binafsi katika Mkoa
  • Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma za Afya
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu katika uandaaji wa mipango ya upambanaji/uzuiaji wa tatizo la Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS)
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uendeshaji wa shughuli zinazohusiana na masuala ya Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS) katika Mkoa
  • Kutoa huduma za Afya/msaada unaohitajika wakati wa milipuko ya magonjwa katika Mkoa
  • Kutoa huduma za kliniki na matibabu kwa wagonjwa wa ndani na nje wanaoletwa kutoka vituo vya Afya/hospitali za mamlaka za Serikali za Mitaa.
  • Kutoa huduma za kitaalamu (utaalamu wa kubobea) za matibabu
  • Kutoa/Kusaidia huduma za kitaalamu na msaada unaohitajika kwa vituo vya Afya na Hospitali za Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa milipuko ya magonjwa yakuambukiza
  • Kutoa huduma za rufaa za maabara na vipimo
  • Kuratibu upatikanaji wa madawa/vifaa tiba kwa ajili ya hospitali.

Utangulizi

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Mkoa wa Dar es Salaam una idadi ya watu takribani 4,369,541 sawa na ongezeko la asilimia 5.6 kwa mwaka, kutokana na ongezeko la kawaida pamoja na wahamiaji wa ndani ya nchi wanaokuja kibiashara na kutafuta maisha mazuri; ambao wanaishi kwenye mitaa ipatayo 452. Idadi hii ya watu inapata huduma za afya kinga na tiba kupitia vituo vya kutolea huduma vya Serikali, Mashirika ya dini na yasiyo ya Kiserikali na Sekta binafsi.

Sekta ya Afya katika ngazi ya Mkoa inaongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa akisaidiwa na Timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa (RHMT). Hadi kufikia mwaka 2013 Mkoa wa Dar es salaam una jumla ya idadi ya zahanati 392 kati ya hizo Zahanati za Serikali ni 89 na za mashirika/watu binafsi ni 303.

Kuna jumla ya Vituo vya Afya 24 kati ya hivyo vituo vya serikali ni 5 na mashirika / watu binafsi ni 27. Hata hivyo, Vituo vya Afya 3 vimeshapandishwa hadhi na kuwa Hospitali (Mnazi Mmoja, Mbagala Rangi Tatu na Sinza)

Aidha, kuna jumla ya Hospitali 36 kati ya hizo 7 ni za Serikali na za watu binafsi ni 29. Kwa ujumla huduma za afya zimeimarika, idadi ya magari ya kubebea wagonjwa (ambulance) ni 19. Ujenzi wa Zahanati unaendelea kwenye maeneo yaliyo pembezoni katika kila Halmashauri zote.

Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke zimepandishwa hadhi kuwa za Rufaa za Mkoa na hivyo kuziwezesha kuwa na Madaktari Bingwa wa magonjwa ya ndani (Internal Medicine) upasuaji, mifupa, watoto na uzazi wapatao kufikia 27. Hii, imesaidia kupunguza rufaa zisizo za lazima kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, Hospitali ya Amana inatoa huduma ya kupima magonjwa ya mfumo wa chakula kwa kutumia kipimo kijulikanacho kama endoscope ambapo awali kilikuwa kikipatikana Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa kutambua mchango wa maambukizi ya VVU katika vifo vinavyotokana na uzazi, Mkoa umezindua mpango wa kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto unaojulikana kama 'option B+' ambao pia unampa mama fursa ya kuanza dawa ya kupunguza makali ya VVU mara tu anapogundulika kuwa na maambukizi ili kuimarisha kinga ya mwili hivyo kuboresha afya na maisha yake kwa ujumla.  
 
Pamoja na jitihada zinazofanyika bado Mkoa unakabiliwa na upungufu wa vituo vya kutolewa huduma za Afya na watumishi ukilinganisha na idadi kubwa ya watu wanaohitaji huduma hiyo kufuatia kasi kubwa ya watu wanaoingia Mkoa wa Dar es Salaam. Mkoa umechukua hatua mbalimbali ikiwemo, kujenga hospitali na vituo vipya vya tiba, kukarabati na kupanua majengo ya kutolea huduma pamoja na kuboresha vyanzo vya mapato ikiwemo kuhamasisha wanachi kujiunga na mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Mkoa unaendelea kuajiri watumishi wenye sifa na ujuzi mbalimbali ili kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Masoko Mapya Yatakayojengwa Washirikishwe Machinga na Viongozi wa Soko

    March 11, 2023
  • RC Makalla Aeleza Kishindo Cha Rais Dkt Samia Suluhu Miaka 2 DSM

    March 10, 2023
  • RC Makalla Atimiza ahadi ya Kuwapeleka Viongozi wa Machinga Taifa Kigali Rwanda

    March 10, 2023
  • RC Makalla Hakuna Fremu Soko la Kariakoo Zilizogawiwa Epukeni Matapeli

    March 26, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akikagua Maendeleo ya Ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa