
-Afanya ukaguzi wa miradi Wilaya ya Kigamboni.
-Atoa maelekezo mahususi kwa niaba ya Waziri wa Nchi OWM-TAMISEMI Prof Shemdoe.
Naibu Waziri wa Nchi OWM TAMISEMI Mhe Reuben Kwagilwa amehitimisha ziara ya kikazi Mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya ya Kigamboni Januari 3, 2026 ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za TARURA kupitia mradi wa DMDP miradi ambayo inatekelezwa kutokana na fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha baada ya ukaguzi huo Mhe Reuben Kwagilwa kwa niaba ya Waziri wa Nchi OWM -TAMISEMI ametoa maelekezo kadhaa kwa Halmashauri katika mikoa yote nchini.
Mosi, Halmashauri ziwe na nidhamu ya makusanyo ya matumizi ya mapato, Utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, Kutekeleza hoja za Mkaguzi wa hesabu za Serikali, na maagizo ya kamati mbalimbali za Bunge pamoja na matumizi sahihi ya mifumo mbalimbali ya TEHAMA.
Vilevile Naibu waziri ameelekeza Halmashauri zipeleke fedha za mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo kwa mujibu wa miongozo, Utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi husika, kuhakikisha maeneo ya Umma yanapimwa kama vile shule na vituo vya Afya, watumishi wafanye kazi kwa bidii na weledi, kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mara kwa mara wa shughuli zinazotekelezwa katika maeneo yao pamoja na kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa Umma.
Mwisho, Naibu Waziri ameagiza Mkoa Dar es Salaam kuhakikisha katika sekta ya elimu kusiwe na uhaba wa meza au kiti ambapo amesema dhamira ya Mhe Rais ni kuona mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia nchi nzima.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa