
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameeleza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi ya BRT phase 4 kuelekea tegeta baada ya kukuta ujenzi huo ukiwa chini ya asilimia 50 wakati unapaswa kuwa umefikia asilimia 65 ambapo ametoa muda wa wiki mbili za matazamio kwa wakandasasi wa mradi huo kuongeza kasi kabla hatua kuanza kuchukiliwa
Akizungumza wakatu anafanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa daraja la mkwajuni na miradi ya ujenji wa barabara wilaya ya kinondoni Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila pamoja na kuridhishwa na ujenzi wa daraja la mkwajuni amesema hayupo tayari kuoma Rais Dkt Samia akitoa fedha nyingi kwenye ujenzi wa barabara za mwendokasi ambazo hazikamiliki kwa wakati.
RC Chalamila amesisitiza kuwa baada ya wiki mbili atazitembelea tena barabara hizo na hatua za kisheria zitachukuliwa endapo hakutakuwa na ongezeko la kasi ya ujenzi huo, hivyo amewataka wakandarasi wanaojenga barabara hiyo kufamya kazi usiku na mchana ( Saa 24)

Akihitimisha ziara hiyo kwenye daraja la mtongani kata ya kunduchi Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa daraja hilo na kufafanua namna ambavyo Rais Dkt Samia ametoa fedha kuboresha miundombinu ndani ya jiji hilo huki akotolea mifano ya daraja la nguva wilayani Kigamboni na mto mzinga wilayani Temeke ambako kote Rais Samia ametoa fedha
Aidha Meneja miradi msaidizi kutoka TANROAD Justin Moshi akatoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa BRT 4 amesema mradi huo ulipaswa kuwa umekamilika hivyo uliongezwa muda lakini bado hatua nyingi hazijakamilika
Akiwa kwenye mradi wa ujenzi wadaraja la Mtongani ambalo lilibomoka kwa mvua Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule ameeleza namna daraja hilo lilivyoleta usumbufu baada ya kubomoka


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa