
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wakazi wa Mkoa huo kupuuza taarifa za uzushi zinazotolewa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii kuwa uchaguzi utakua na vurugu badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura kwani Mkoa huo uko Salama sana wakati wote kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari RC Chalamila amesema Mkoa huo una wapiga kura zaidi milioni nne na kwamba tayari tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeshakamilisha miundombinu kwa ajili ya wananchi kupigia kura ndani ya Mkoa huo hivyo amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura bila kuhofia usalama wao kwani vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri kuimarisha amani
Aidha RC Chalamila amevionya vikundi vinavyotishia kuvuruga wakati wa uchaguzi kupitia mitandao ya kijamii na kubainisha kuwa vyombo vya dola viko macho kuchukua hatua dhidi ya mtu anayebainika kufanya au kutaka kuleta vurugu na amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola endapo kuna viashiria vya vurugu
Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mwananchi anapata nafasi ya kutumia haki yake ya kikatiba ya kupiga kura bila hofu wala vurugu kwakua Serikali inatambua kuwa suala hilo ni haki ya kikatiba
Pamoja na mambo mengine Chalamila amevitaka vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi bila kufanya upotoshaji kwani vyombo vya habari ni muhimuli muhimu ambao ni kiunganishi kati ya wananchi na Serikali yao ambapo ametumia pia nafasi hiyo kuwataka viongozi kuanzia ngazi ya mitaa kulinda miundombinu ya Serikali ikiwemo ya umeme na barabara za mwendokasi ambapo amisisitiza barabara hizo kutotumiwa na vyombo vingine vya usafiri

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa