• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKALLA: ASIMAMIA ZOEZI LA KUSAINI MKATABA WA LISHE KWA WAKUU WA WILAYA

Posted on: October 26th, 2022


 -Awataka Wakuu wa Wilaya kusimamia vema utekelezaji wa viashiria 14 vilivyopo katika Mkataba huo

- Aagiza Mkataba huo kushuka kwenye kata mpaka mitaa

 -Ataka changamoto zote kufanyiwa kazi Mara moja

-Amewasihi wazazi wote wenye watoto mashuleni kushirikiana na Kamati za shule  ili kusaidia watoto kupata chakula

-RMO asema Dsm inaendelea kufanya vema pia katika lishe, chanjo ya  UVIKO na kuchukua tahadhari ya Ebola

-Afisa Lishe wa Mkoa akiri Dsm kujipanga zaidi na kuhakikisha kila Halmashauri kufika asilimia 95

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 26, Oktoba 2022 amesimamia zoezi la kusaini MKATABA wa Lishe kwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huo katika Ukumbi wa Anatoglo Jijini Dar es Salaam

RC Makalla amewataka Wakuu hao wa Wilaya kusimamia kikamilifu utekelezaji wa viashiria 14 vilivyopo katika Mkataba huo ambavyo ni pamoja na watoto kupatiwa chakula mashuleni, wakina mama wajawazito kuhudhuria clinic ipasavyo na kupatiwa madini joto, watoto kupatiwa matone ya vitamins A, Watoto wenye utapiamlo mkali kupatiwa Huduma vituoni, na utoaji wa fedha ipasavyo kwa ajili ya Afua za lishe

Mkuu wa Mkoa ameelekeza Mkataba huo kushuka kwenye kata mpaka kwenye mitaa kwani ni  wa wananchi na kusisitiza kuwa Leo yeye ameanza na Wakuu wa Wilaya na wao wakafanye hivyo mpaka ufike mitaani

Aidha, RC Makalla ameagiza changamoto zote zikiwemo za utengaji wa fedha za afua za lishe, Utoajia wa Elimu ya Lishe kwa wananchi, chakula kwa wanafunzi zifanyiwe kazi Mara moja

Mhe. Makalla amewasihi wazazi wote wenye watoto mashuleni kushirikiana na Kamati za shule ili kusaidia watoto hao kupata chakula kwani chakula kinasaidia uwepo wa watoto mashuleni, kuongeza usikivu, ufanisi na kupunguza utoro kwa watoto Hali inayopelekea kuchochea ufaulu

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dr. Rashid Mfaume amesema Dar es Salaam imeendelea kufanya vizuri katika suala la lishe, utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 na kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Ebola

Naye Afisa Lishe Mkoa Bi. Janeth Stanley amekiri kuendelea kujipanga zaidi ili kuhakikisha Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kila kiashiria kufikia asilimia 95 na sio chini ya hapo

Ikumbukwe kuwa Rais wa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ndio muasisi wa Jambo hili toka akiwa Makamu wa Rais na amesaini na Wakuu wa Mikoa Mkataba wa Miaka 8 kwa sasa

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa