-Asema Mkoa unajumla ya mitaa 564 ambayo itashiriki uchaguzi huo
-Vituo vya kupiga kura katika mitaa vimeongezwa ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Wilaya ya Ilala amewataka wananchi hususani wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kupiga kura Novemba 27,2024 ili kupata kiongozi atakayewaletea maendeleo.
Aidha RC chalamila amesema vituo vya uchaguzi vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni, Mkoa unajumla ya mitaa 564 ambayo itashiriki katika uchaguzi huo pia Mkoa umejipanga vizuri katika kuhakikisha unawafikia watu wengi zaidi kwa kuongeza vituo vya kupiga kura katika mitaa.
Vilele amevitaka vyombo vya Habari kutoa taarifa sahihi za uchaguzi na kuhamasisha wananchi kupiga kura.
Sanjari na hilo RC Chalamila amewataka wananchi pamoja na vyama vya siasa kushiriki uchaguzi huo kwa kuzingatia 4R za Rais Samia yenye maana ya Maridhiano, Ustamilivu, Mageuzi na Kujenga upya "Lazima tujenge siasa zenye ustamilivu, siasa ambayo tunakaa pamoja na kuepuka siasa za Chuki" Alisema RC Chalamila
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa