Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 16, 2024 ameungana na wakazi wa Mkoa huo pamoja na viongozi mashuhuri kuaga Mwili wa Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu) katika eneo la Hospitali ya JWTZ Lugalo.
Aidha Meja Jenerali Mbuge alikutwa na umauti Oktoba 12, 2024 Nchini India katika Hospitali ya Apollo ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Hivyo kwa mujibu wa ratiba heshima za mwisho za marehemu zimetolewa leo katika Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo baadaye mwili huo unasafirishwa kwenda Kyabakari Mkoani Mara kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 17, 2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa