Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kudumisha amani wanaposherehekea sikukuu ya mwaka mpya huku akisisitiza kuendelea kumshukuru Mungu kwa baraka zake katika kipindi cha mwaka uliopita 2025
Akizungumza leo Disemba 31, 2025 na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam wakati akitoa salam za mwaka mpya 2026 RC Chalamila amesema Mkoa huo umeendelea kuwa salama tena sana huku akisisitiza kuwa Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kusimamia uwepo wa amani nchini kwa umakini mkubwa lakini kila mtu anapaswa kulinda amani na kuepuka taharuki za mafataki bila kibali cha polisi na uchomaji wa mataili wakati wa kusherehekea mwaka mpya 2026
Aidha RC Chalamila amezungumzia hatua kubwa za kimaendeleo ambazo Mkoa umeendelea kutekeleza ikiwemo ujenzi wa baranara na madaraja unaoendelea kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa huo ikiwemo barabara ya Jangwani ambayo imekuwa na changamoto nyingi hasa nyakati wa mvua ambapo amewataka wakandarasi wa ujenzi huo kufanya kazi usiku na mchana ili mradi ukamilike kwa wakati pia akizungumzia ujenzi wa barabara kupitia mradi wa DMDP.
Akizungumzia changamoyo ya upungufu wa maji kwenye Mkoa huo kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, RC Chalamila amesema kwa sasa mvua zimeanza kunyesha kiwango cha maji kwenye mto Ruvu kimeogezeka vilevile Serikali ya Dkt Samia imeendelea kutafuta suluhu ya kudumu ya uhaba wa maji kwa kujenga bwawa kubwa la kisasa la kidunda ili kumaliza changamoto ya maji huku kukiwa na mpango mwingine kabambe wa kutumia mto Rufiji kusambaza maji jijini humo
Aidha amezungumzia suala la umeme ambapo amesema serikali Mkoani humo imaendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme pia amezungumzia mikakati ya mkoa huo kupokea wanafunzi zaidi ya 95,323 wanaotakiwa kuwa shuleni kidato cha kwanza mwezi januari 2026 pamoja na wanafumzi wa shule za awali na msingi huku akisisitiza suala la kutokuwepo kwa michango isiyo ya lazima mashuleni.
Sanjari na hayo amezungumzia mpango wa bima ya afya kwa wote kama ambavyo Rais Dkt Samia ameelekeza huku akisisitiza suala la wananchi kutopata usumbufu wa kuchukua miili ya wapendwa wao wanapotangulia mbele ya haki wakiwa Hospitalini
RC Chalamila vilevile amezungumzia changamoto iliyojitokeza Oktoba 29 ya matukio ya uvinjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu ambapo amesema Serikali imaendelea kurejesha huduma muhimu za kijamii zilizoharibiwa huku akielekeza wamamchi kushirikiana na Serikali kudumisha amani na kuwataka viongozi wa dini kudumisha amani

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa