-Aongoza Bonanza la kuhamasisha jamii kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27,2024
-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kuendelea kulinda amani ambayo ni Tunu ya Taifa.
Katibu wa Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila ameongoza mamia ya wakazi wa Mkoa huo katika Bonanza la kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Akitoa hotuba wakati wa Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Katibu Tawala wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo na na kulinda Amani ambayo ni Tunu ya Taifa kwa umahiri mkubwa ambapo alisemaBonanza hili, limehusisha michezo ya aina mbalimbali ikiwemo matembezi ya Polepole ambayo yalianzia Uwanja wa Uhuru hadi Mwembe Yanga Pia Michezo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, mchezo wa kuvuta Kamba na mingine mingi.
Aidha Dkt Toba alisema Kupitia Bonanza hili viongozi wa Serikali,vyama vya Siasa wamepata fursa ya kujumuika na wananchi mbalimbali wa Mkoa, kubadilishana mawazo pia kujadili masuala yanayohusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi huo.
Sanjari na hilo imekuwa fursa adhimu kwa kila mmoja aliyeshiriki Bonanza hili ambapo wananchi wamejipatia elimu kuhusu haki zao za kisheria na ushiriki wao katika uchaguzi wa kidemokrasia ili kuchagua viongozi wenye uwezo wa kusimamia maendeleo na kuunganisha jamii zao.
Vilevile Dkt Toba alisema Ofisi ya Rais -TAMISEMI inaendelea kusisitiza kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni sehemu muhimu ya kukuza demokrasia na maendeleo katika jamii,na hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunashiriki kupiga kura kwa wingi na kwa Amani.
Mwisho Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Nguvila alikabidhi tuzo na zawadi mbalimbali kwa washindi wa Bonanza hilo “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi,Jitokeze Kushiriki Uchaguzi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa