Mkoa wa Dar es Salaam una Halmashauri za Manispaa tano (5) ambazo ni Ilala, Kinondoni na Temeke, Ubungo, Kigamboni na Halmashauri ya Jiji. Halmashauri za Manispaa pamoja na Halmashauri ya Jiji zinaongozwa na Wastahiki Mameya ambao ni Wenyeviti wa Halmashauri, kwa kushirikiana na Wakurugenzi ambao ni Watendaji wakuu wa Halmashauri husika.
Halmashauri za Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Halmashauri ya Jiji hutoa huduma za kiuchumi zikiwepo Kilimo, Mifugo, Misitu, Uvuvi, Miundombinu, Huduma za jamii kama Afya, Maji, Elimu, Maeneo ya burudani, Mazishi, Mipangomiji, Kutunza mazingira, Ustawi wa jamii, Ushirika na mambo mengine yanayoihusu jamii na Taifa kwa ujumla.
Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982). Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa na sheria hiyo ni kama ifuatavyo:-
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa