Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea kituo kikuu cha kuzalisha umeme TANESCO kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam pamoja na vituo vya kupoza umeme vya mabibo na Mbagala ikiwa ni katika kukagua uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya umeme ambapo amewahakikishia wananchi kuwa suala la kukatika kwa umeme jijini humo linakwenda kuwa historia.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema Mkoa huo pekee Serikali imewekeza takriban shilingi Trilioni 1.3 kwenye sekta ya umeme hivyo suala la kukatika umeme kwa sasa sio kwa sababu za upungufu wa umeme bali ni maboresho tu ya miundombinu hususani baada ya Rais Dkt Samia kukamilisha ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwl Nyerere
Aidha RC Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa huo kushirikiana na Serikali kulinda miundombinu ya shirika la umeme, isiharibiwe ili kuendelea kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwani shughuli zote za kiuchumi na uwekezaji zinahitaji uimara kwenye sekta ya umeme
Vilevile RC Chalamila ameendelea kuwakumbusha wakazi wa Mkoa huo na watanzania waliojitokeza kwenye ziara hiyo kuwa Octoba 29 mwaka huu ni siku ya uchaguzi hivyo kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze kupiga kura kwa kwa amani huku akiwatahadharisha wote wenye nia ya kuleta vurugu kuwa Serikali haitowavumilia
Naye Naibu Mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme nchini TANESCO kwa upande wa usambazaji umeme Mhandisi Atanasius Nangali ameeleza namna serikali Mkoani humo ilivyoongeza uwekezaji kwenye uzalishaji umeme huku Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando aliposhiriki ziara hiyo amesema uwekezaji wa umeme unaofanyika umekuwa na manufaa makubwa kwenye kuboresha maisha na kuongeza ajira kwa vijana
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa