-Ataka mikopo inayotolewa na Serikali kwa makundi hayo itolewe bila rushwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ameelekeza mikopo inayotolewa na Serikali kwa makundi mbalimbali ya wajasiriamali na wafanyabiashara ikiwemo wanawake vijana na watu wenye ulemavu itolewe kwa uadilifu bila uwepo wa vitendo vya rushwa kwani yapo malalamiko kuwa waombaji mikopo wamekuwa hawapatiwi fedha kamili kama walivyoomba badala yale kulazimika kutoa shukrani kupitia fedha hiyo
Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha makundi maalumu ya mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Mama lishe,Baba lishe, vijana,Wanawake,Bodaboda, Machinga na wadau mbalimbali, Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema fedha za mikopo zinatolewa na Rais ili kuyawezesha makundi maalumu lakini ipo changamoto ya wakopaji kulazimika kutoa shukrani kupitia fedha hizo jambo ambalo huathiri kazi zao
Aidha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza mikakati ya Rais Dkt Samia kuimarisha usafiri wa umma jijini humo kwa kuijenga miumdombinu bora na kuruhusu kampuni binafsi kuanza kutoa huduma ya usafiri wa mwendokasi ambao sasa umeanza kuimarika huku pia akisisitiza wananchi kujitokeza kushiriki kupiga kura Octoba 29,2025
Sanjari na hayo katika kukabiliana na changamoto ya ajira Waziri Mkuu Majaliwa ameshauri vijana kusoma kwa kizingatia kada yenye uhitaji mkubwa ndani ya jamii lakini pia kusoma taaluma ambazo zinaruhusu vijana kujiajiri
Awali kabla ya kumkaribisha Waziri mkuu,Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makumdi maalumu Dkt Doroth Gwajima amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia haijamuacha mtu ama kikundi cha watu kwenye mpango wa maendeleo kwani amekuwa akiwezesha makundi yote ili watimize malengo yao
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameeleza namna ambavyo Serikali chini ya Rais Dkt Samia imekuwa ikiwawezesha wafanyabiashara kwa kuimarisha miundombinu ya barabara, madaraja uwepo wa umeme wa uhakika pamoja na kuboresha usafiri wa mwendokasi ambao ulikua ukilalamikiwa na amewahakikishia usalama wakazi wa jiji hilo kipindi cha uchaguzi.
Nao baadhi ya wadau na wataalamu walioshiriki Mkutano huo wameishukuru Serikali kwa maelekezo ya namna bora ya utoaji mikopo ili iwanufaishe wafanyabiashara wadogo badala ya mikopo hiyo kuwa ni adhabu kwa wafanyabiashara na wameahidi kushiriki kupiga kura oktona 29,2025
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa