Utangulizi
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ipo kati ya Latitudo 6 na 7 kusini mwa Ikweta na kati ya Longitudo 39 na 40 Mashariki. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina eneo la kilomita za mraba 210 ambapo zaidi ya asilimia 75% ya eneo hilo la Manispaa ya Ilala ni eneo la mji.
Manispaa ya Ilala imepakana na Manispaa za Kinondoni na Temeke kwa upande wa Kaskazini na Kusini, Mkoa wa Pwani kwa upande wa Magharibi na Bahari ya Hindi katika ukanda wa Pwani wenye urefu Kilomita 10 kwa upande wa Mashariki.
Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya iliyofanyika Agost 2012, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina jumla ya wakazi wapatao 1,220,611, ambapo idadi ya Wanaume ni 595,928 na na wanawake ni 624,683
Utawala
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imegawanyika katika Tarafa tatu (3) ambazo ni Ukonga , Ilala , na Kariakoo . ambapo ina jumla ya Kata Thelathini na tano (35) zikiwa na jumla ya Mitaa mia moja na hamsini na tatu (153)
Aidha Halmashauri ya Manispaa ina Majimbo matatu (3) ya Uchaguzi ambayo ni Ilala, Ukonga na Segerea.
Mstahiki Meya ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Manispaa ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa. Manispaa inaongozwa na Baraza la Madiwani.
Shughuli kuu za Wakazi
Shughuli muhimu za kiuchumi katika Manispaa ya Ilala ni biashara, viwanda, kilimo na uvuvi pamoja na huduma za kiuchumi na kijamii. Pato la wastani la mkazi wa Manispaa ya Ilala ni sh.489, 204.00 kwa mwaka.
kujua zaiadi kuhusu Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bofya hapa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa