• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda ya Kutembelea Miradi Mikubwa ya DAWASA

Posted on: June 9th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda amefanya ziara ya kutembelea Miradi Mikubwa  inayotekelezwa na Serikali na kusimamiwa na DAWASA tarehe 08/06/2017 kwa lengo la  kujionea kazi kubwa inayofanywa na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Awali Mhe. Paul Makonda akiwa katika Ofisi ya DAWASA Makao Makuu alipokea taarifa kutoka kwa Maafisa Watendaji wakuu wa DAWASA na DAWASCO kuhusu uwepo wa taasisi hizo, majukumu yao, mafanikio na changamoto zilizopo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa baada ya kupokea taarifa hizo alianza ziara ya kutembelea miradi hiyo ambapo alianza kwa kujionea mradi wa Tangi la Maji maeneo ya Kibamba na kupata maelezo ya mradi huo halafu akaelekea katika mradi wa Ruvu juu Darajani ambapo hapo alijionea mitambo ya uzalishaji  wa maji sambamba na kukagua kituo kipya cha kusukuma Majighafi na kupata maelezo ya uendeshaji wa kituo hicho.

Aidha, Mkuu wa Mkoa alitembelea pia Mradi wa Maji Ruvu Juu na kukagua Mitambo Mipya ya kutibu maji na Kupata maelezo ya uendeshwaji wa mitambo hiyo, halikadhalika alimalizia kwa kutembelea Mitambo mipya ya usafishaji,kutibu na kusukuma Maji ya Ruvu Chini na kukagua mitambo hiyo ikiwemo kupata maelezo ya upanuzi wa Mitambo hiyo.

Baada ya hapo Mhe. Paul Makonda alipata nafasi ya kuongea ambapo alisema kuwa amefurahishwa sana na juhudi kubwa zinazofanywa na watendaji wa Sekta hiyo ya Maji katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa nafasi ya kipekee alimshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwajibikaji wake na kuwateua watu wanaoweza kufanya kazi kikamilifu akiwemo Waziri wa Maji, Katibu Mkuu wake na Hatimae kutupatia DAWASA na ikapelekea kupatikana kwa DAWASCO ili kuhakikisha watu wanapata majisafi.

Mhe. Paul Makonda amesema kuwa kwa upande wa Ruvu juu wameongeza uzalishaji wa maji kwa kiwango cha lita Millioni 196 zinazozalishwa kwa siku aidha Ruvu chini ambapo nao wanazalisha zaidi ya lita Millioni 270 ambapo yakijumlishwa haya maji ni mengi sana na kupelekea kupunguza kero ya maji katika Jiji letu la Dar es Salaam. Aidha, mkakati wa kuendelea kupunguza maji yanayopotea ni mkubwa. Wakati huo huo mfumo wa maji taka unaendelea kuudhibitiwa ili kuondoa kabisa tatizo la mfumo huo unaosababisha magongwa mbalimbali.

Mhe. Paul Makonda aliwataka wananchi wote wasiokuwa na huduma ya maji katika maeneo yao kufika katika Ofisi za DAWASCO kujisajili ili kuwekewa miundombinu ya maji na kisha kupata maji na kuwekewa utaratibu mzuri wa kuyalipia maji hayo kupitia Ankara zao

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Injinia Romanus Mwang’ingo alieleza kuwa wamempitisha Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na DAWASA ili kuona hali halisi na anaamini kuwa ndani ya mwaka mmoja ujao kwa wale waliokuwa hawana maji watapata maji na wale waliokuwa hawana mtandao wa maji pia wataupata kwani mkandarasi wa kusambaza maji yupo kazini.

Vile vile Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Injinia Cyprian Luhemeje alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda namsafara wake kwa kuwatembelea na kujionea hali halisi sambamba na kueleza kuwa mpango mkakati umewekwa wa kuhakikisha ndani ya mwaka mmoja watafika asilimia 85 na pamoja na kupunguza ya usambazaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa yakagua Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Temeke

    May 07, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Maadhimisho ya Mei-Mosi Dar es Salaam.

    May 01, 2025
  • Dkt Hussein Ally Mwinyi Aweka Jiwe la Msingi Barabara ya Kiibada, Mwasonga-Kimbiji

    April 25, 2025
  • RC Chalamila Dar ni Salama Aeleza Mafaniko na Mipango ya Maendeleo ya Mkoa

    April 18, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa