Akifungua mafunzo hayo ya mfumo wa manunuzi ya Umma wa kielektroniki NeST Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Aman Mafuru amesema lengo la mafunzo ni kujifunza jinsi ya kutumia mfumo mpya na kuhakikisha Taasisi zote nunuzi zinatumia mfumo huu katika manunuzi yote yanayotumia fedha za Umma
Aidha Mhandisi Mafuru amesema faida za mfumo wa NeST ni kuongeza Uwazi, Ushindani na Usawa katika Shughuli za Ununuzi hivyo kupunguza mianya ya Rushwa na kupata thamani halisi ya fedha katika Ununuzi wa Umma.
Mfumo wa TANePS utafika ukomo wa manunuzi ifikapo Septemba 30, 2023 hivyo mfumo mpya utaanza kutumika rasmi Octoba 1, 2023, Taasisi nunuzi hazitaruhusiwa kufanya ununuzi wa umma nje ya mfumo wa NeST. Taasisi nunuzi ambayo itafanya ununuzi wowote bila kutumia mfumo wa NeST itakua imetenda kosa na hivyo Afisa masuhuli wa Taasisi husika atachukuliwa hatua zinazostahili kwa mujibu wa Sheria.
Vilevile amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa na kuiwezesha wizara ya Fedha kwa kushirikiana na PPRA kujenga mfumo huu hivyo amewataka washiriki wote wa mafunzo hayo kujifunza kwa bidii ili baada ya mafunzo haya kwenda kufundisha idara tumizi ndani ya Halmashauri zao kabla au ifikapo Septemba 15, 2023
Mwisho Mafunzo hayo ni ya siku tano (5) ambayo yameanza leo Agosti 29,2023 yanatarajiwa kumalizika Octoba 2, 2023 yanawahusisha Wataalam kutoka Sekretarieti ya Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Halmashauri zote tano (5) za Mkoa huo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa