Mkuu wa Mkoa Mhe Amos Makalla akishiriki usafi wa pamoja februari 26, 2022 kariakoo Ilala Jijini Dar es Salaam.
Na, Bornwell Kapinga IO- DSM
Jiji la Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu Taifa la Tanzania lipate Uhuru limetajwa kuwa Jiji la Sita kwa Usafi Afrika kufuatia taarifa ya kitafiti iliyotolewa na “Africa Tours”, chanzo hicho kimebainisha Majiji 12 Safi katika Afrika “Top 12 cleanest Cities in Africa” ambapo Jiji namba 1. Kigali – Rwanda, 2. Port Louis- Mauritius, 3. Cape Town- South Africa, 4. Tunis- Tunisia, 5.Windhoek-Namibia, 6. Dar es Salaam –Tanzania, 7. Gaborone- Botswana, 8. Algiers- Algeria, 9. Nairobi- Kenya, 10. Libreville- Gabon, 11. Kumasi-Ghana, na 12. Asmara- Elitrea
Kwa upande wa Afrika Mashariki ukizingatia mtiririko uliotolewa na “Afica Tour” unakuta Jiji la Dar es Salaam ni la Pili kwa Usafi kwa hiyo wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa Ujumla wanapaswa kujipongeza na kuweka jitihada za kwenda mbali Zaidi ikibidi kufikia nafasi ya kwanza
Nimelazimika kuandika Makala hii nikilenga kubainisha Mkakati wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam Uliozinduliwa na Mhe Amos Makalla ambao unachagizwa na Kauli mbiu ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM kwa hakika ndio umepelekea Jiji la Dar es salaam kushika nafasi ya Sita kwa Usafi miongoni mwa majiji 12 Safi katika Afrika.
Wana Dar es Salaam wanapaswa kutambua Ukiongelea Tanzania unaongelea Jiji la Dar es Salaam kwa kuwa Dar es Salaam ndilo jiji la kibiashara, ndio lango la Nchi, Bandari kubwa, Uwekezaji mkubwa na Wageni wa nchi mbalimbali Duniani wanaotoka na kuingia, hata kama wanaenda sehemu nyingine lazima watapitia Dar es Salaam,
Kwa mantiki hiyo wakazi wa Dar es Salaam wanapaswa kumuunga mkono RC Makalla ambaye ndiye anaye mwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika Mkoa huu.
Mkuu wa Mkoa Mhe Amos Makalla katika kuhakikisha anaacha alama katika Mkoa wa Dar es Salaam amekuwa na mikakati na mbinu nyingi katika suala la usafi, alianza na kuwapanga vizuri wafanya biashara wadogo alimaarufu “Wamachinga” hapo awali kulikuwepo na utitiri wa biashara holela kila kona ya mkoa, ilifikikia hata barabara za watembea kwa miguu zilikuwa hazipitiki, vibanda vilijengwa ovyo kila sehemu, shughuli za kina mama lishe nazo zilikuwa zinafanyika kiholela hata kwenye taasisi za umma nako kulizingirwa na wamachinga kwa mfano IFM na CBE hali hiyo ilikuwa chanzo kikubwa cha uchafu katika Jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa pasipo kutumia nguvu aliwataka wafanyabiashara hao kwenda katika maeneo rasmi yaliyotengwa kwa ajili yao katika kila wilaya za mkoa, huku akitumia mbinu ya ushawishi na kuwaelimisha hatimaye zoezi la kuwapanga vizuri machinga likafanikiwa.
Kilichofuata ilikuwa ni usafi kwa kuwa maeneo mengi waliyohama yalikuwa machafu ndipo akaandaa muongozo au kitabu ambacho kilibainisha Mkakati wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira katika Mkoa, kukiwa na kauli Mbiu SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM, kampeni ambayo aliizindua rasmi Disemba 4, 2021 akidhamiria kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa Safi wakati wote.
Mambo muhimu yaliyoanishwa kuhusu Kampeni ya Usafi kwanza kabisa Udhibiti wa biashara holela, pili Udhibiti wa Uchafuzi wa mazingira (Utupaji wa taka), Usafishaji wa Jiji/kufanya Usafi, Uzoaji wa Taka zilizozalishwa katika kila mitaa au kata, Usafirishaji wa taka na Uteketezaji, Mkakati wa Upandaji miti,Uendelezaji wa bustani na maeneo ya Umma ya Kupumzika, na ushirikishwaji wa wadau katika kutekeleza mapango.
Mambo hayo ambayo RC Makalla ameyaainisha ikiwa ni mkakati katika Kampeni ya Usafi ndio utekelezaji wake umefanyika na matokeo yameonekana, Wana Dar es Salaam sasa wanapaswa kuendelea kumuunga mkono ili nafasi ambayo jiji kwa sasa limeshika katika usafi lisirudi nyuma badala yake liende mbele zaidi ikiwezekana Jiji la Dar es Salaa liwe la Kwanza Afrika kwa Usafi.
Aidha katika kufurahia ushindi uliopatikana katika kipindi kifupi ni wakati muafaka wa kutafakari na kuijitathimini kwa kuhakikisha hakuna mfanyabiashara anayefanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi, kudhibiti utupaji taka ovyo, kufanya usafi iwe ni tabia lakini kila ifikapo tarehe ya mwisho wa mwezi Jamii ijenge utamaduni wa kufanya usafi wa pamoja, kuboresha mzingira ya uzoaji taka zinazozalishwa, usafirishwaji wa taka na uteketezaji katika madampo ya kisasa, vilevile kupanda miti na kuendeleza bustani na maeneo ya Umma ya kupumzika bila kusahau wadau mbalimbali wa mazingira washiriki katika mpango Usafi kwa Ujumla wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa