• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Ugawaji wa Apron

Posted on: June 7th, 2017

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na WHO imegawa  jumla ya  Apron 257 zenye thamani ya Tshs 2,929,800/= kwa Mama lishe na Baba lishe wa Soko la Buguruni – Ilala na Sterlio – Temeke leo asubuhi kufuatia  juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali ya Mkoa katika kupambana na ugonjwa hatari wa kipindupindu.

Zoezi hilo la ugawaji wa Apron lilipokelewa vema katika Masoko yote kwa wahusika kujitokeza kwa wingi ili waweze  kupokea Apron zao kwa ajili ya kudumisha usafi katika maeneo yao ya kazi.

Awali Afisa Afya wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Dennis Kamzolah aliwaambia Mama lishe na Baba lishe wa Soko la Buguruni kuwa maeneo yao yanapaswa kuwa masafi kwani kinyume chake ugonjwa hatari wa kipindupindu utatokea na ukitokea utasababisha vifo vya watu sambamba na kufunga biashara hivyo itakuwa hasara pia kwa upande wao.Aliwataka kuweka chakula chao katika mazingira safi na salama. Aidha, kuwawekea misingi ya usafi wateja wao pindi wanapokuja kwa kunawa katika maji ya moto na sabuni, kuwa na kapeti la kuwekea vyombo, Dustibins n.k.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buguruni Bw. Adam Fugame aliishukuru Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na WHO kwa kugawa Apron hizo kwa Mama lishe na Baba Lishe wa soko lake na kuwataka kina Mama lishe na Baba lishe kuzingatia yote wanayopaswa kuyazingatia ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na uchafu.

Katika Soko la Sterlio – Temeke Kaimu Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bi. Rehema S. Ally aliwaeleza Mama lishe na Baba lishe waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kupewa Apron kuwa katika utekelezaji wa majukumu yao msingi mkubwa ni Usafi kwani bila kuzingatia hilo itapelekea kutokea kwa magonjwa mbalimbali katika biashara zao. Hivyo aliwataka kuzingatia kanuni zote za Afya.

Akitoa shukrani kwa Serikali ya Mkoa na WHO Baba lishe Bw. Mussa D. Jumbe amesema wamepokea Apron kwa furaha na wanaamini itakuwa ni chachu kwao kwa ajili ya kuwahamasisha wazidi kuzingatia suala la usafi.


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa