Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea 'Garage' ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kukagua maendeleo ya ukarabati na ubadilishaji mwonekano wa Magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi yaliyosafirishwa mkoani Moshi hivi karibuni.
Akiwa katika Garage hiyo Mheshimiwa Makonda amejionea magari hayo yakiwa katika hatua mbalimbali za utengenezaji ambapo ameomba uongozi wa kampuni hiyo kukamilisha ukarabati wa magari hayo kwa wakati iliyaweze kuongezea ulinzi na usalama jijini Dar es salaam.
Aidha Makonda amesema kuwa anataka kubadili mwonekano wa jeshi la polisi Mkoa wa Dar es salaam kwa kuhakikisha magari ya polisi yanakuwa na hali nzuri itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa uufanisi kwa kuyabadili magari hayo kuwa kama yale ya Askari wa umoja wa mataifa.
*"Hakuna kitu kinachoninyima usingizi kama pale Mwananchi anapohitaji polisi wafike mahala pa tukio na polisi hawafiki, na kufanya hali ya amani kutoweka na wakati huohuo polisi wanataka kufanya kazi yao ila wanashindwa kutokana na uhaba wa vifaa.Hii ndiyo sababu ninahangaika ili siku moja Dar es Salam iwe na amani hata kufikia hatua ya watu kufanya Biashara zao masaa 24na kutembea kwa amani muda wote."*alisema Makonda.
*Nimepata Pikipiki 200, baiskeli 500 na kuweza kutengeneza magari haya 56 kuwa na viwango vya kimataifa kama magari ya Umoja wa Mataifa (U.N) yanavyoonekana,yaani kwenye gari ya doria itaweza kuwa na maafisa wa polisi tisa kwa nyuma,ambao watatu watakuwa kushoto na watatu kulia mwa gari hiyo huku wawili wakiwa nyuma ya gari hiyo na mmoja akiwa amesimama mbele na silaha kubwa."*aliiongeza Makonda.
Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, (DCP) Lucas Mkondya amempongeza Mheshimiwa Makonda kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha askari wanafanya kizi katika mazingira mazuri.
Nae mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya RSA Ltd inayokarabati magari hayo Bwana Varinder Bhamra amesema kuwa watahakikisha ukarabati wa magari hayo unamalizika kwa wakati huku akieleza kuwa wataendelea kushirikiana na mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam bega kwa bega.
Ikumbukwe kuwa Mnamo Mwezi 14 mwaka huu jumla ya magari mabovu ya polisi 26 yalisafirishwa kutoka Dar es salaam kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kufanyiwa ukarabati na kubadili mwonekano.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa