• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Serikali yazindua rasmi tovuti za Mikoa 26 ya Tanzania bara na Mamlaka za Serikali za Mitaa 185

Posted on: March 27th, 2017

Historia imeandikwa nchini Tanzania tarehe 27 Machi, 2017 mara baada ya Serikali kuzindua rasmi tovuti za Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Mamlaka za Serikali za Mitaa 185. Hafla ya uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Simbachawene (Mb), na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), na Mkurugenzi Msaidizi wa USAID Tanzania, Tim Donnay, ambao ndio wafadhili wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). Waziri Simbachawene katika hotuba yake ameishukuru na kuipongeza Shirika la Msaada la watu wa Marekani, USAID kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma “PS3”, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wakala ya Serikali Mtandao kwa kushirikiana pamoja katika kusanifu mfumo wa pamoja “Government Website Framework” ambao umesaidia kutengeneza na kusimamia tovuti za Serikali zenye kiwango na muonekano mmoja ambao ni rahisi wakati wa kufanya maboresho ya pamoja, rahisi na rafiki kwa mtumiaji pindi watakapokuwa wanazitembelea. Mhe. Simbachawene ameendelea kufafanua kwamba suala la upatikanaji habari na taarifa mbalimbali ni takwa la kisheria na kikatiba, hivyo basi viongozi wa taasisi za umma wana wajibu wa kuhakikisha kuwa taarifa mbalimbali za utekelezaji Serikalini zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati. Katika hatua nyingine, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), ameeleza kuwa tovuti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ni njia rahisi na bora ya kuwafikishia wananchi taarifa za utekelezaji Serikalini. Amefafanua kwamba, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha sheria mbili zinazowapa wananchi haki ya kupata taarifa na habari.

Mhe. Mwakyembe, amewakumbusha maofisa habari na TEHAMA wajibu wao wa kuzihudumia tovuti na kuhakikisha kuwa taarifa sahihi zinawafikia wananchi kwa uwazi na kwa wakati na pia ametoa wito kwa viongozi wa taasisi za umma kuwapa ushirikiano maofisa habari na TEHAMA wanapohitaji taarifa za kuwekwa kwenye tovuti kwani mafanikio na uhai wa tovuti hizo hayatamtegemea mtu mmoja.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa