• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA: HAKUNA BOMOA BOMOA YA KARNE DAR ES SALAAM

Posted on: October 23rd, 2017


Ndugu zangu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Naomba kuwatoa hofu, Mimi Paul Makonda nikiwa Mkuu wenu wa Mkoa na mtumishi wa serikali ya awamu ya tano, napenda kuwataarifu kwamba Serikali hii inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli HAIVUNJI Nyumba ya mtu Bali inaendelea kurasimisha Makazi kama ambavyo ilifanya kimara kwa kuwapatia Hati elfu Sita (6000) Wananchi waliokuwa wamejenga kwenye makazi yasiyo rasmi, jitihada zinaendelea na ndivyo itakavyofanyika tarehe 27/10/2017 kwa Wananchi waliojenga katika maeneo ya Makongo juu.

Naomba niseme, na kama nimemuelewa vizuri alichokisema Mhe William Lukuvi ambae ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni kuwa wananchi wasiendelee kujenga bila vibali vya ujenzi jambo ambalo linawanyima haki yao ya kukopeshwa, kulipa kodi ya majengo, na mwishoni kuwa na Miji isiyopangwa vizuri.

Naomba kukiri kuwa apo awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa vibali vya ujenzi jambo ambalo haliwezi kuwa Adhabu kwa Wananchi waliojenga miaka ya nyuma iliyopita kwani ilifika hatua mwananchi ana Hati ya Kiwanja chake na amekamikisha michoro kwa Mujibu wa Sheria na ana fedha za kuanza Ujenzi kwa ajili ya Makazi ya kuishi, unakuta Mwananchi huyo analazimika kufuatilia Manispaa kwa zaidi ya miaka miwili mpaka mitatu bila kupata kibali cha ujenzi na hata akipata kibali baada ya miaka Mitatu na kuanza ujenzi, unakuta ndani ya muda mfupi watakuja baadhi ya watu wa OSHA kumsimamisha kwa madai hawana taarifa ya ujenzi jambo linalotengeneza mianya ya Rushwa, akimalizana na watu wa OSHA Wanakuja baadhi ya watu wa kikosi cha zimamoto (fire) nao inabidi atafute utaratibu wa kumalizana nao, jambo linalokera wananchi na kuwafanya wakose hamasa ya Kutafuta vibali vya ujenzi na hatimae kujenga kiholela.

Kutokana na jambo hili, baadhi ya watu wasiowaaminifu wanatumia mwanya huu kuvamia maeneo ya watu na kujenga Kiholela na kuibua Migogoro Mikubwa ya Ardhi.

TULICHOFANYA KAMA MKOA

Kutokana na sababu hizo na changamoto nilizozielezea hapo juu, serikali ya Mkoa tulifanya kikao na wataalamu wa Ardhi na nikatoa maelekezo kuwa vitengo vyote nane vinanavyohusika na Utoaji wa vibali vya ujenzi VINAPASWA kuwa na mfumo Mmoja wa mawasiliano (one stop center) ili Mwananchi atakapoomba kibali cha ujenzi Idara zote nane zifikiwe kwa wakati Mmoja na kupunguza usumbufu wa Mwananchi kwenda kufuatilia vibali na wakati mwingine unaambiwa wahusika hawapo.

Ili mfumo huo uanze kufanya kazi wataalamu wangu walihitaji vitendea kazi ambavyo nimewawezesha vifaa hivyo zikiwemo Computer Hamsini (50) katika manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka kutoa vibali ndani ya mwezi Mmoja tangu kupokea maombi kutoka kwa Mwananchi tofauti na awali ambapo Mwananchi alikuwa akichukua muda wa miaka miwili kufuatilia kibali cha ujenzi, lengo Likiwa kuwawezesha wananchi kufuata Sheria ili kuendana na Mpango wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na makazi Chini ya Mhe William Lukuvi katika kuhakikisha tunapanga miji yetu.

Kwa maelezo haya mafupi, Naomba niseme kwenye Mkoa wa Dar es Salaam HAPATAKUWA na bomoa bomoa ya KARNE wala Nyumba ya mtu kuvunjwa ISIPOKUWA wananchi wanaojenga sasa ni vyema wakafuata utaratibu kama alivyoelekeza Mhe William Lukuvi waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, ili kuepuka kuvunjiwa Nyumba ambayo umeijenga kwa jasho jingi, na kujinyima uku ukikesha ili utimize ndoto ya kuwa na makazi bora.

Niwatakie kazi njema, na kwa pamoja tushirikiane katika Kupanga na kuendeleza Mkoa wetu wa Dar es Salaam kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa na vizazi vyetu.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa