Kufutia tahadhari ya mvua kubwa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa nchini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka wananchi kuanza kuchukuwa tahadhari ya mapema ilikukabiliana na majanga ya mafuriko huku akiwataka wakazi wa mabondeni kuhama.
RC Makonda amesema ujenzi holela na tabia ya watu kutupa taka kwenye mifereji na mito ndio imekuwa chanzo kikubwa cha mafuriko hivyo amewahimiza wananchi kuacha mara moja tabia hiyo.
Aidha RC Makonda ametoa siku saba kwa wakala wa barabara za Mjini na Vijijini TARURA kuhakikisha wanaziba viraka katika barabara kwakuwa vimekuwa usumbufu na kero kwa watumiaji wa barabara huku akiwaagiza TANROAD kusafisha miundombinu ya Mito,mitaro na madaraja yaliyoziba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa