• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA AKUTANA NA UGENI WA WALIMU 18 KUTOKA MAREKANI

Posted on: July 13th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea wageni 18 kutoka Nchini Marekani ambao ni walimu wa shule za  Msingi, Sekondari na Vyuo  waliokuja Nchini kujifunza Utamaduni wa Tanzania.

Ugeni huu ni kutokana na mahusiano aliyoyajenga kipindi akiwa nchini Marekani wakati wa likizo yake mwishoni mwa mwaka jana.

Katika mazungumzo ya pamoja na Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda amewasilisha kwa walimu hao kutoka majimbo mbalimbali nchini Marekani maombi mawili, ambayo ni Ujenzi wa Maktaba ya kisasa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam, kwani hitaji la kusoma kwa wananchi wa kawaida ni kubwa na kutokana na uhaba wa maktaba rafiki kwa kada zote hapa jijini.

Maktaba hii pia itasaidia upanuzi wa uelewa wa mambo mbalimbali  katika nyanja za uchumi, siasa, kilimo, tehama na teknolojia za kisasa katika sekta za madini, misitu ya asili, mito, maziwa na wanyama adimu wanaopatikana nchini Tanzania tu.

Lengo ni kumuwezesha mkazi wa Dar es salaam kuwa na uelewa mpana wa mambo na kujadiri mambo ya kitaifa na kidunia kwa utafiti mkubwa zaidi.

Na pia uanzishwaji wa programu maalum ya kuleta walimu wa ngazi mbalimbali kutoka nchini Marekani kwa ajili ya kufundisha shule za Mkoa wa Dar es salaam. Hitaji la walimu hawa ni jibu la changamoto kubwa ya ukosefu wa walimu wa sayansi na Tehama nchini.

Maombi hayo mawili yamepokelewa na kikundi hicho cha walimu na kuongeza kuwa wapo tayari kuanza ujenzi wa maktaba hiyo endapo ofisi ya Mkoa itatoa eneo la ujenzi wa Maktaba hiyo, lakini pia watatoa jumla ya nakala 59,000 ya vitabu mbalimbali vya kisasa kwa ajili ya maktaba hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mh. Makonda alisema, “Mimi ningependa Wanafunzi wa Mkoa wa Dar es salaam wajue Dunia inaendaje, na mkakati tulionao na ndugu zangu hawa 18 ambao wengine ni Mabosi wakubwa Marekani ni kuwa na umoja wa kuwa na utaratibu wa kuletewa walimu kutoka nchini humo, hii itatusaidia sana”.

Kwa upande wake kiongozi wa msafara huo Dr. Fredoline Anunobi amesema kuwa watahakikisha wanajenga Maktaba hiyo ya kijamii kwa wakati ili kuwezesha wananchi kupata huduma muhimu ya elimu muhimu na pamoja na kuwaleta walimu wa masomo ya sayansi na tehama katika mkoa wa Dar es salaam.

Mratibu wa Mipango kutoka Albany Community Charter School Shannari Akosua kutoka Marekani alimshukuru Mkuu wa Mkoa kuwakaribisha vizuri na kueleza kuwa wamefurahi kuwepo katika mkoa wa Dar es salaam na kwa  namna ya kipekee ambavyo Mkoa unajenga mahusiano na wadau mbalimbali wa maendeleo na kuahidi kushawishi taasisi nyingi zaidi kutoka nchini Marekani kufanya kazi na Mh. Makonda katika kuendeleza mkoa wa Dar es salaam.

Bi. Shannari alisisitiza kuwa watakuwa mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vya utalii viliopo nchini sambamba na lugha adhimu ya kiswahili ambayo ni moja ya mambo waliyojifunza kutoka hapa nchini.


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa