Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo July 12 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32.
RC Makonda amesema kuwa ndani ya siku tano ambazo mwenge ulikuwa jijini Dar es salaam umefanikiwa kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 36 ya maendeleo kwenye wilaya zote tano.
Aidha RC Makonda amewashukuru wananchi wa Dar es salaam kwa ushirikiano mkubwa walioonyesha tangu siku mwenge ulipoingia hadi leo alipoukabidhi kwa mkoa wa Pwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa