- NIDA Textile waomba serikali kupitia TRA kudhibiti vitenge vya magendo.
- Uzalishaji umeshuka kutoka mita miolini 8 mpaka milioni 4.
- RC Asema serikali itaendelea kuchukua hatua Za kulinda viwanda vya ndani Na ameagiza TRA kuchukua hatua Za haraka
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Mamlaka ya mapato TRA kudhibiti uingiaji wa Bidhaa za Magendo kwakuwa zinachangia kudorora kwa uzalishaji wa viwanda vya ndani na kupelekea kufa.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara kwenye Kiwanda Cha NIDA Textiles Mills Ltd Baada ya kupokea malalamiko ya ongezeko la Bidhaa za Magendo ikiwemo Vitenge, Mashuka na kanga ambapo kwa mujibu wa Kiwanda kilikuwa kikizalisha Mita Milioni 8 za vitenge kwa mwezi lakini Baada ya kushamiri vitenge vya Magendo uzalishaji umeshuka mpaka Mita Milioni 4
Kutokana na Hilo RC Makalla amewahakikishia Wawekezaji Wenye viwanda kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya Biashara ikiwa ni pamoja na kusimama kidete kudhibiti Bidhaa za Magendo.
Aidha RC Makalla amekipongeza Kiwanda hicho kwa uzalishaji wa *Bidhaa zenye ubora jambo linaloitangaza Nchi kimataifa.
Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda Cha NIDA Textiles Mills Ltd Mohamed Honelo mbali na kumshukuru RC Makalla kwa kuchukuwa hatua za haraka kuwatembelea Baada ya kupokea malalamiko pia wameahidi kuendelea kuzalisha Bidhaa zenye ubora
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa