• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Njia ya Watembea Kwa Miguu na "Road Reserve" Dar , Lazima Ziwe Wazi

Posted on: September 9th, 2021

Mhe Amos Makalla akiongea na Machinga mtaa wa Msimbazi Kariakoo Mapema leo.

- Asema Kufanya biashara holela  barabarani ni kukiuka Sheria na  haki za watembea kwa miguu

- Amtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala kukaa na uongozi wa Machinga Kariakoo Septemba 13, 2021

- Asisitiza anawajibu wa kusimamia Sheria na Usalama wa wananchi wa Dar es Salaam

- Asema wamachinga ni watu muhimu katika nchi hii lakini ni vizuri kufuata utaratibu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla mapema leo Septemba 9,2021 amezuru eneo la msimbazi karibu na Jengo la Club ya Simba Kariakoo Ilala, Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika eneo hilo Mhe Makalla alipata wasaa wa kutembea kwa miguu katika eno hilo kujionea namna wafanyabiashara wadogo walivyopanga biashara zao katika miundombinu ya barabara ya DART na kuwaathiri watembea kwa miguu kupata ajali wengine kupoteza maisha.

Mhe Makalla akiongea na hadhara iliyokusanyika kumsikiliza ametoa tamko kuwa kuanzia sasa njia za watembea kwa miguu na "road reserve" ni lazima ziwe wazi katika Mkoa wa Dar es Salaam kufanya biashara holela barabarani ni kukiuka sheria na haki za watembea kwa miguu.

" Ni vema kila mwananchi kuheshimu sheria na haki ya mwingine na mimi Mkuu wa Mkoa moja ya jukumu langu ni kusimamia sheria na haki za wananchi " Alisema *Mhe Makalla*

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amesma biashara holela barabarani katika eneo la Kariokoo zinasababisha ajali na watu kupoteza maisha jana tu kuna watu wamegongwa na mwendokasi na wengine kupoteza maisha, nitoe pole kwa familia lakini hii hali sasa ifike mwisho.

Aidha amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na timu yake Jumatatu Septemba 13, 2021 kukaa na uongozi wa Machinga Kariakoo na kuja na mpango wa kuwaondoa machinga katika miundombinu ya barabara ya DART Msimbazi pasipo kuathiri biashara zao ikiwezekana kubainisha sehemu ya kuwapeleka au kuwa na siku maalum za kufunga barabara fulani kuruhusu machinga kufanya biashara.

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan inawapenda wafanyabiashara wadogo hivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam hakuna machinga atakayekosa sehemu ya kufanya biashara  awataka kufuata utaratibu.

Kiongozi wa Machinga Kariakoo Ndg  Lusinde amekiri kuwepo kwa biashara holela yeye na viongozi wenzake wako tayari kukaa na uongozi kwa wa Wilaya ili kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo


 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa