-Asema Vyandarua vitagawiwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi DSM, takribani 785,548
-Asisitiza watoto wote wenye umri kuanzia miaka 0 - 5 kupatiwa Chanjo ya POLIO
- Atoa Rai juu ya matumizi sahihi ya Vyandarua na Umuhimu wa watoto kupatiwa Chanjo ya POLIO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo April 14 amezindua rasmi Kampeni ya Ugawaji Vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi pamoja na Chanjo ya POLIO kwa watoto wenye umri kuanzia 0-5 katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika Ukumbi wa mikutano Anatoglo Mnazimmoja Ilala Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa, Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Wazee, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakurugenzi,na Wajumbe wote wa kamati ya huduma za Afya ya Msingi
RC Makalla wakati akizindua Ugawaji wa Vyandarua amesema Vyandarua ni *Salaama vimetengenezwa Tanzania tusipotoshwe, tuvitumie Vyandarua hivyo lakini tusisahau kuchukua tafadhari zote dhidi ya Ugonjwa wa malaria ikiwemo kufanya usafi kuzuia mazalia ya mbu bahati nzuri tayari tuna Kampeni ya Usafi jambo lililoko mbele yetu ni kuendeleza Kampeni hiyo.
Aidha RC Makalla amebainisha kuwa tayari nchi jirani Malawi wamebaini mtu mwenye maambukizi ya Ugonjwa wa POLIO, Tanzania hatuwezi kuwa salama ni vema kuuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuwapatia Chanjo ya POLIO watoto wote wenye umri kuanzia miaka 0-5
Vilevile wananchi waendelee kujipatia chanjo zingine ikiwemo ya Uviko-19 kutokana na ukweli kuwa ukichanja una asilimia kubwa ya kupona ukiugua hivyo "Ujanja ni Kuchanja" Alisema RC Makalla
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa DSM Dkt Rashid Mfaume akitoa taarifa ya awali amesema Kiasi cha Malaria katika Mkoa ni chini ya 1% hali sio mbaya sana lakini ni vyema tukashiriki vizuri katika zoezi la Ugawaji vyandarua kwa wanafunzi na kuhakikisha matumizi sahihi ya vyandarua hivyo.
Kwa upande wa Chanjo ya POLIO watoto watakaopatiwa ni kuanzia umri wa miaka 0-5, hivyo kwa kuwa nchi Jirani Malawi tayari wameshabaini uwepo wa mtu mwenye maambukizi ya POLIO Tanzania lazima tuchukue tafadhari ikiwemo kuwapatia watoto Chanjo hiyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa