- Akoshwa na mwamko Mkubwa wa Wananchi kufanya usafi na kuwahimiza kuongeza jitiada.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA. Amos Makalla amezindua kampeni ya Usafi wa mtaa kwa Mtaa Wilaya ya Ubungo ambapo amewaelekeza Viongozi kuanzia ngazi ya mtaa mpaka Wilaya kuhakikisha suala la Usafi ni agenda muhimu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyokwenda sambamba na Usafi wa pamoja Wilaya ya Ubungo eneo la Mlimani City, RC Makalla ameonyesha kufurahishwa na *mwamko wa Wananchi kufanya usafi.
Aidha RC Makalla ameendelea kupiga marufuku ufanyaji Biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ikiwemo kwenye Barabara za watembea kwa miguu, Maeneo ya hifadhi ya Barabara, chini ya mitaro, mbele ya maduka mbele ya taasisi za umma.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema ifikapo March 12 atawasafirisha Viongozi wa Machinga Taifa kwenda Jijini Kigali Nchini Rwanda kwaajili ya Mafunzo ya namna wenzetu wamefanikiwa kwenye usafi Kisha watafuata Wakuu wa Wilaya.
Miongoni mwa washiriki wa Zoezi Hilo ni pamoja na Wakuu wa Wilaya Ubungo na Kinondoni, Wabunge wa Kibamba na Ubungo, Madiwani, Watendaji wa Mkoa na Wilaya, Viongozi wa mtaa, Viongozi wa Machinga Taifa na Mkoa, Bank ya NMB, Chama Cha Mapinduzi CCM na Wadau mbalimbali wa Maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa