RC Makalla Akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wapya wa Wilaya za DSM
M - Mapato
K - Kero za Wananchi
U - Ulinzi na Usalama
U - Usafi wa Mazingira
U - Ufuatiliaji Miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya waliohamishiwa Vituo vya Kazi Mkoani humo kuhakikisha Wanafanya majukumu Yao kwa Weledi na ufanisi Ili kumsaidia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliewaamini na kuwateua.
RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao kazi na Wakuu wa Wilaya waliohamishiwa Mkoani humo na wale waliokuwepo awali na kuhamishiwa Vituo vipya vya kazi ambapo pia amewakabidhi Vitabu vya Mwongozo wa Mpangokazi wa kuwapanga vizuri Wafanyabiashara wadogowadogo na mkakati wa usafi Dar es salaam.
Miongoni mwa Wakuu hao wa Wilaya ni pamoja na Edward Mpogolo Mkuu wa Wilaya ya Ilala akitokea Wilaya ya Same, Halima Bulembo Wilaya ya Kigamboni akitokea Muheza, Hashim Komba Wilaya ya Ubungo akitokea Nachingwea, Mwanahamisi Mukunda Wilaya ya Temeke akitokea Bahi na Saadi Mtambule Wilaya ya Kinondoni akitokea Mufindi.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, RC Makalla amewasisitiza kufanya usimamizi thabiti wa ukusanyaji wa mapato na utatuzi wa kero na changamoto za Wananchi.
Aidha RC Makalla amewaelekeza kusimamia kikamilifu suala la Ulinzi na usalama, usafi wa mazingira na kufanya ufuatiliaji na Wa Miradi ya maendeleo.
Pamoja na hayo RC Makalla amewasisitiza kufanya kazi kwa kuzingatia Utekelezaji wa *ilani ya uchaguzi ya CCM, Maagizo ya Viongozi wa Juu wa Serikali na Sera na mwelekeo wa CCM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa