• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Aridhishwa na Hali ya Maji Ruvu Juu na Chini

Posted on: July 15th, 2022

- Atoa wito Kwa Wananchi kulinda vyanzo vya maji Na kuombea mvua Za Vuli zinyeshe ili maji yasipungue

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewahakikishia Wakazi wa Mkoa huo kuwa Hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji Safi ni nzuri Kufuatia DAWASA kuchukuwa hatua stahiki za kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji msimu wa kiangazi ikiwemo Ujenzi wa Mabwawa ya kutunza Maji.

RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara kwenye Vyanzo vya Maji Ruvu juu na Chini akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge pamoja na wajumbe wa Kamati za ulinzi na usalama za Mkoa wa Dar es salaam na Pwani.

Katika ziara hiyo RC Makalla amejionea kina Cha Maji Ruvu juu kikiwa Mita 16 na Ruvu Chini Mita 4.2 Ambapo kwa mujibu wa DAWASA kiwango Cha Maji Cha Sasa kinaweza kutuvusha salama kipindi Cha Kiangazi.

Kutokana na Hali ya upatikanaji wa Maji kuwa ya kuridhisha *RC Makalla* ameelekeza *Kamati ya Ulinzi na usalama na Mamlaka ya Bonde la Wami/Ruvu* kufanya *Operesheni* za Mara kwa mara na kuwachukulia hatua watu watakaobainika *kuchepusha maji bila Vibali.*

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi wa Dini kufanya Dua za kuombea mvua za Vuli zinyeshe ili yasitokee majanga ya ukame Kama yaliyotokea mwaka Jana.

Pamoja na hayo RC Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitiada za dhati anazofanya kuboresha sekta ya Maji kupitia miradi Mikubwa ya usambazaji wa maji pembezoni Mwa mji na kuwapongeza DAWASA kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kusimamia Vizuri miradi ya maji.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DAWASA Eng. Cyprian Luhemeja amesema Mamlaka hiyo inaendelea kufanya kila jitihada za kuhakikisha kiasi Cha Maji kilichopo kinalindwa na kudhibiti upotevu wa maji.

Aidha Mhandisi. Luhemeja amewataka Wananchi kutunza na kulinda Vyanzo vya Maji ili kuwepo na upatikanaji wa maji ya uhakika.

Itakumbukwa kuwa mnamo mwaka Jana maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam yalikumbwa na tatizo la uhaba wa maji Kutokana na ukame uliosababishwa na kutokunyesha kwa mvua za Vuli na ndio maana siku ya Leo Wakuu wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani pamoja na Kamati za ulinzi na usalama wameona ni vyema kuchukuwa hatua za kukabiliana na Changamoto hiyo


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa