- Uongozi Hospitali ya Muhimbili wasema kurudi kwa machinga eneo la Muhimbili ni eneo hatarishi
- RC Makalla atangaza eneo hilo ni hatarishi wamachinga wabaki maeneo waliyopangiwa
-Ahamasisha wananchi kushiriki usafi katika maeneo yao
RC Makalla ameongoza kufanya usafi Hospitali ya Muhimbili eneo la stendi leo Octoba 28,2022 akiwa pamoja na Uongozi wa Hospitali hiyo, Wadau wa Usafi, na Wananchi wanaozunguka katika eneo hilo
Aidha Uongozi wa Hospitali hiyo chini ya Mtendaji Mkuu Prof Mohamed Janabi wamesema wamachinga wamerudi katika eneo ambalo ni hatarishi ambapo kuendelea kufanya shughuli zao katika eneo hilo ni rahisi kupata magonjwa na kwenda kueneza kwa watu wengine
Kwa hiyo kutokana na wamachinga kurudi katika eneo hilo ambalo ni hatarishi RC Makalla ametangaza wamachinga wabaki katika maeneo waliyopangiwa na Serikali ambayo ni rasmi
Sambamba na hilo RC Makalla amehamasisha Wananchi kushiriki usafi katika maeneo yao ili kuendana na kampeni endelevu ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam Usafi husaidia kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu
Hata hivyo RC Makalla amepokea vifaa vya usafi kutoka Kampuni ya Uniliver na shilingi milioni moja kutoka kwa mdau wa usafi wa eneo la standi ya Muhimbili familia ya Mbaga fedha ambayo ameelekeza inunue vifaa vya usafi pia
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili *Prof Mohamed Janabi* amemhakikishia mkuu wa Mkoa kuendeleza usafi katika eneo la Hospitali na amethibitisha kitaalamu kuwa eneo la stendi ni hatarishi hivyo wanafanyabiashara wadogo (wamachinga) wasifanye biashara eneo hilo
kumbukwe kuwa RC Makalla ameshiriki Usafi wa mwisho wa mwezi katika eneo hilo ikiwa ni muendelezo wa utaratibu aliojiwekea wa kujumuika na jamii kufanya Usafi kila mwisho wa mwezi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa