• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Amtaka Mkandarasi wa Visima vya Kigamboni Kurudi Site Mara moja

Posted on: May 9th, 2023

 

- Ni baada ya mradi kusuasua na mkandarasi kutoonekana kazini kwa muda mrefu

- Mpaka Sasa mkandarasi amepokea Shilingi bilioni 54, kati ya Visima 20 ni 7 pekee vimekamilika.

- Awataka DAWASA Kuwasilisha ndani ya siku 7 mpango wa upatikanaji maji wakati wa Ukame

- Atoa Wiki Moja kwa DAWASA wampatie mpangokazi wa ujenzi wa miundombinu ya kupokea Maji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya Serengeti anaetekeleza Mradi wa Visima vya Maji Kimbiji na Mpela kurudi site mara Moja baada ya mkandarasi huyo kusuasua na kuingia mitini.

CPA, Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Ziara ya kukagua kama mradi huo unaendelea au umesimama na kuthibitisha pasipokuwa na shaka kuwa Kazi zimesimama kwa muda mrefu.

Kutokana na Hilo, CPA Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo kuweka kambi kwenye Miradi hiyo na kuhakikisha kazi usafishaji wa Visima inafanyikwa kwa Kasi Ili vikamilike mapema.

Aidha CPA, Makalla ametoa muda wa wiki Moja kwa Bodi na Menejimenti ya DAWASA kumkabidhi mpangokazi wa ujenzi wa miundombinu ya kupokea Maji kutoka kwenye visima hivyo na kuyapeleka kwenye bomba Kuu.

Lengo la CPA Makalla ni kuona DAWASA inakuwa na mbadala wa Maji ya Dharura yatakayosaidia kipindi Cha miezi ya November na December ambapo kunakuwa na ukame Unaopelekea mgao wa Maji na Mkuu wa Mkoa anaamini visima vya Kimbiji na Mpela vinaweza Kusaidia kupunguza makali ya mgao.

Pamoja na hayo CPA, Makalla amewaelekeza DAWASA kuhakikisha Wananchi wa Kata ya Kisarawe Two wanafikiwa na huduma ya Maji.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo na Kaimu mtendaji mkuu wa DAWASA Eng.Shaban Mkwanywe kwa pamoja wamesema utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa utaanza Mara Moja.

*Mradi wa Visima vya Maji Kimbiji na Mpela unahusisha visima 20 ambapo kati ya hivyo visima 7 pekee ndio vimekamilika jambo ambalo RC Makalla hakubaliani nalo sababu mradi ulitegemewa kukamilika tokea mwaka 2014.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa