• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Kunenge Atembelea Miradi na Kutaka Ikamilike kwaWakati

Posted on: September 17th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge leo tarehe 17 Septemba, 2020 amefanya ziara ya kukagua miradi iliyopo katika Wilaya za Kinondoni, Ubungo, na Ilala na kutaka miradi hiyo ikamilike kwa wakati uliopangwa.

Awali Mhe. Kunenge alikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Tegeta Nyuki yenye urefu wa kilometa 1.06 inayosimamiwa na Tarura na kujengwa na kampuni ya CMG Construction iliyopo katika Wilaya ya Kinondoni ambapo alimtaka mkandarasi wa mradi huo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kwani amekua akisuasua kumaliza mradi huo licha ya kuongezewa muda.

“Wakandarasi wasipofanya kwa wakati waliopewa wanaongeza kero kwa wananchi, hivyo naagiza mradi huu uwe umekamilika kwa kiwango cha rami na mitaro mizuri ilfikapo Oktoba mwishoni”. Aliagiza RC Kunenge

Baada ya hapo msafara wa Mhe. Mkuu wa Mkoa ulielekea katika ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Madale kuelekea Wazo yenye urefu wa Kilomita 6 inayogharimu kiasi cha Tshilingi Billioni 9.9 ambapo Mkuu huyo wa Mkoa alifurahishwa na juhudi za usimamizi na ujenzi wa mradi huo ambapo alisema mkandarasi wa mradi huo yupo ndani ya muda na ujenzi huo unaenda vizuri. Alimtaka mkandarasi huyo pia asibweteke bali aukamilishe mradi huo ndani ya muda uliopangwa.

Aidha, RC Kunenge  pia ametembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Stand Mpya ya mabasi ya kisasa ya Mbezi Louis ambayo ujenzi wake umefika 80% na inagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 56 ambapo ameonyesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi ilipofikia.

Mwisho kabisa RC Kunenge ametembelea ujenzi wa Daraja la Ulongoni A lililopo Kata ya Gongolamboto ambalo ujenzi wake unagharimu Shilingi Bilioni 4.3 na unatarajia kukamilika ifikapo Aprili, 2021 na Ujenzi wa Daraja la Ulongoni B ambapo amewahimiza wakandarasi kuongeza juhudi kwa kufanya kazi usiku na mchana  ili ujenzi ukamilike ndani ya Muda uliopangwa ili kupunguza kero walizokuwa wakizipata wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Ulongoni A Bw. Ibrahimu Hamisi alitoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwatengea kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kwani changamoto katika madaraja hayo ni kubwa hasa katika upitaji wa watu, magari, pikipiki na bajaji.

“Mchakato unavyoendelea tunaamini inaweza ikawa faraja kwetu” Alisema Mwenyekiti wa Ulongoni A Bw. Ibrahimu Hamisi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa