-Asema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu inatarajia kuadhimisha miaka 20 Februari 17, 2025.
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya bodi ya mikopo ya wanzafunzi wa elimu ya juu februari 17 mwaka huu ambapo Rais Dkt Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wadau mbalimbali kushiriki maadhimisho hayo pia amewataka wahitimu wa vyuo walionufaika na mikopo inayotolewa na Bodi kufanya marejesho ili kutoa fursa kwa wanafunzi wengine kuweza kunufaika
Akizungumza leo Feb 13, 2025 ofisini kwake Ilala Boma-Jijini Dar es salaam na waandiahi wa habari RC Chalamila amesema bodi ya mikopo ya elimu ya juu inaadhimisha miongo miwili yaani miaka 20 tangu kuanzishwa kwake ikiwa imenufaisha zaidi ya wahitimu 830,000 kwa kuwapatia mkopo hivyo ni muhimu kwa wahitimu walio katika ajira rasmi na waliojiajiri kufanya marejesho
Aidha RC Chalamila amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu imeongeza bajeti ya fedha kwenye bodi hiyo kutoka shilingi bilioni miatano sabini kwa mwaka wa fedha 2021-2022 hadi kufikia shilingi bilioni mia saba themanini na saba kwa mwaka 2024-2025 na kwamba kwa mwaka huu zaidi ya wanafunzi laki mbili na na elfu arobaini na saba wananufaika na mikopo hiyo hivyo ni muhimu kufanya marejesho
Sambamba na hilo RC Chalamila amezungumzia maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo ya mikopo ambapo amesema maadhimisho hayo yameanza februari 10 kwa maonesho ya huduma za bodi hiyo yatakayodumu hadi februari 14 kwenye mikoa 7 ya kikanda ambayo ni Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dar es salaam, Mtwara pamoja na Zanzibar lengo likiwa ni kukutana ni kutanua wigo wa kutoa huduma hiyo.
Vilevile RC Chalamila amesema kuwa Alfajiri ya februari 15 kutakua na mbio za pole yaani joging zitakazoongozwa na Rais wa Zanzibar Dokta Hussein Mwinyi kuanzia viwanja vya farasi Oesterbay na kilele cha maadhimisho hayo kitakua februari 17 ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa JNICC
Mwisho kilele hicho kitahudhuriwa pia na wageni kutoka mataifa mbalimbali kutoka bara Asia,South America,Ulaya na bara la Afrika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa