-Asema Rais Samia amefanya uwekezaji katika sekta ya maji zaidi ya Bilioni 490.
-Mitambo ya bilioni 6 kufungwa ili kumaliza changamoto ya kukosekana kwa maji
-Aitaka DAWASA kusimamia kwa karibu upotevu wa maji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 2, 2024 amefanya ziara katika ofisi za makao makuu DAWASA Jijini humo akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama Mkoa, wakuu wa Wilaya zote za Mkoa, pamoja na wataalam wengine.
RC Chalamila amesema lengo la ziara yake katika mamlaka hiyo ni kutokana na malalamiko ya watu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa huo kuhusu kukosekana kwa maji ambapo amewatoa hofu wananchi kuwa tayari Serikali imeshachukua hatua za haraka kupunguza changamoto ya ukosefu wa maji kwa kuagiza baadhi ya mitambo ya zaidi ya bilioni 6 itakayosaidia uchujaji na usafirishaji wa maji kutoka kule kwenye chanjo kwenda kwa wananchi.
Mhe Chalamila amesema malalamiko ni ya muda mfupi tu ndani ya kipindi cha miezi 3 mitambo itakuwa tayari imeshafungwa na huduma ya maji kurejea kama kawaida. " Rais Dkt Samia amefanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya bilioni 490 katika sekta ya maji Mkoa wa DSM matarajio yetu malalamiko yatakuwa machache" Alisisitiza Mhe Chalamila.
Kwa upande wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire ametoa shukrani kwa Rais Dkt Samia kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya maji ambapo ameaidi kutekeleza kwa weledi mkubwa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kwa masilahi mapana ya wananchi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa