-Azindua tamasha maalum la Bata la Disemba na Heineken
-Asema tamasha likwenda sambamba na kuhamasisha wananchi matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amezindua tamasha kabambe maarufu kwa jina la ' Bata la Disemba' ambalo limeandaliwa na wazalishaji wa kinywaji cha Heineken kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
RC Chalamila akizindua tamasha hilo katika ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini humo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Novemba 27,2024. " Piga Kura Siku moja, kula bada siku 3 akiwa na maana kuwa watu watumie vizuri siku ya tarehe 27, 2024 kuhakikisha wanapiga kura baada ya hapo wasubiri Bata la Disemba katika viwanja vya Leaders kuanzia Disemba 6 hadi 8, 2024" Alisema Chalamila.
Aidha RC Chalamila amesema tamasha hilo litakwenda sambamba na kuhamasisha wananchi kutumia Nishati safi ya kupikia ambapo mitungi zaidi ya 1000 itagawiwa kwa kina mama lishe na Baba lishe.
Ifahamike kuwa kupitia Canival hiyo mitaa yote ya Mkoa wa DSM itachangamshwa na muziki, chakula, burudani na bila shaka kwa mpango ulioratibiwa na bia bora zaidi ya Heineken.
Canival hilo sio tu litaleta furaha kwa wakazi lakini pia litavutia wageni kutoka kote, kanda na kwingineko ikivutia zaidi wahudhuriaji 10,000 kutoka kote Afrika Mashariki
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa