• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Marufuku Mabaunsa Kutumika Kutoa Watu Meneo Yenye Migogoro DSM.

Posted on: September 24th, 2025

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo Kufuatia ukiukwaji wa sheria na vitendo vya ukatili vilivyofanywa na Mabaunsa dhidi ya wapangaji wa Bi Alice Paskali Haule kwenye nyumba yenye mgogoro iliyopo Msasani Beach jijini Dar es Salaam ambapo ameagiza kuanzia sasa mabaunsa wasitumike kutoa watu kwenye maeneo yenye migogoro badala yake madalali wa mahakama watumie jeshi la polisi ambao wanaweledi wa kufanya kazi hiyo

Mgogoro wa nyumba hiyo ambayo ni kiwanja namba 891 unahusisha mke wa marehemu Justis Lugaibula bi Alice Paskali Haule na bwana Muhamed Mustafa Yusufali ambae anaonekana alinunua nyumba hiyo kutoka kwa marehemu Justis Lugaibula enzi za uhai wake bila kumshirikisha mkewe

Akizungumza jijini Dar es salaam RC Chalamila ametoa agizo hilo leo septemba 24 alipofika katika nyumba hiyo msasani beach jijini humo baada ya jana septemba 23 kuona video zikionesha mabaunsa wakitumia nguvu kubwa na ukiukwaji wa haki za binadamu kuwaondosha watu waishio kwenye nyumba hiyo yenye mgogoro.

Aidha Chalamila ameagiza nyumba hiyo kutotumika na upande wowote wa mgogoro hadi hapo mgogoro utakapomalizika ambapo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya kinondoni kuuunda kamati ya wataalamu ikiwemo jeshi la polisi, ofisi ya kamishina wa ardhi na wataalamu wengine ambapo ameitaka kamati hiyo na pande zote mbili za mgogoro kufika ofisini kwake ijumaa Septemba 26

Hata hivyo akizungumzia mgogoro huo bi Alice Pascal Haule ambaye ni mke wa marehemu Justis Lugaibula amesema yeye na mumewe walinunua nyumba hiyo mwaka 2008 lakini amekuwa akipata usumbufu kutoka mabaunsa wakidai kuwa Muhamed Mustafa Yusufali aliuziwa nyumba hiyo na mumewe wakati yeye anafahamu walikopeshana pesa na sio kuuziwa nyumba

Naye mwakilishi wa Muhamed Mustafa Yusufali ambae yupo safarini Bi Hajja Mungula amesema yeye anafahamu kuwa Muhamed alinunua nyumba hiyo mwaka 2011 kutoka kwa Marehemu Justis Lugaibula ambaye ni mume wa Alice kwa shilingi milioni 262 na kwamba Alice aliweka alama yake ya dole gumba kwenye nyaraka ya mauziano

Kwa upande wa Kamishina msaidizi wa ardhi Mkoa wa Dar es salaam Bw Shukrani Kyando ameeleza namna ambavyo nyaraka za nyumba hiyo zilivyokuwa zikibadilishwa kila inapouzwa na kusema kuwa kwa mujibu wa nyaraka zilizopo sasa nyumba hiyo aliuziwa Muhamed Mutafa Yusufali na hivyo hati inasoma jina lake huku mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule akisisitiza changamoto ya uwepo wa mabaunsa wasio na weledi wa kazi katika wilaya hiyo


Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 July 17, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA WA DARASA LA SABA MEI, 2025 July 18, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEADHIBIWA-MAKUMBUSHO SEKONDARI September 23, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEADHIBIWA-MAKUMBUSHO SEKONDARI September 23, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Marufuku Mabaunsa Kutumika Kutoa Watu Meneo Yenye Migogoro DSM.

    September 24, 2025
  • RAS - DSM Sports Club yapata ushindi wa pili katika Mchezo wa Draft

    September 22, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mawili kwa Wakuu wa Wilaya ya Ubungo,Kigamboni na Gari moja kwa Golikipa wa Taifa Stars

    September 22, 2025
  • RC Chalamila Atoa Salaam za Pole kufuatia vifo 4 vya Masista wa Kanisa Katoriki

    September 19, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa