Wakati Tanzania ikiwa inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Marais wa Afrika unaotarajia kufanyika Januari 27 na 28 mwaka huu kujadili masuala ya Nishati Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea maeneo muhimu kuelekea mkutano huo na kueleza kuwa maandalizi yamekamilika kwa zaidi ya aailimia 90.
Akizungumza leo Januari 20,2024 jijini Dar es salaam alipofanya ziara kuanzia eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK Nyerere akikagua barabara na usafi wa mazingira hadi kwenye kumbi za Karimjee na ukumbi wa kimataifa wa JNICC RC Chalamila amesema maandalizi yapo hatua za mwisho na kwamba Serikali mkoani humo inakamilisha kufunga taa za kisasa ili kuhakikisha jiji hilo linakua na mwanga wa kutosha
Aidha RC Chalamila amesisitiza suala la usafi na kupendezesha Jiji hilo ambapo amewataka wananchi kuhakikisha usafi unafanyika sio kipindi hiki cha ugeni bali iwe ni utamaduni wa kila siku vilevile kuwepo na bustani za miti na maua ili Mkoa huo uendelee kuwa kivutio kwa mikutano mbalimbali ya kimataifa na uwekezaji
Sambamba na hilo RC Chalamila ameongeza kuwa baadhi ya barabara zitafungwa ili zitumiwe na wafanyabiashsara na wajasiriamali wa kitanzania ili kuonesha bidhaa mbalimbali za kiutamaduni zinazoitambulisha Tanzania kwenye mataifa mbalimbali yanayoshiriki mkutano huo huku akiweka msisitizo kwenye suala la kuendelea kudumisha amani na utulivu kwa nchi ili Tanzania iendelee kuwa kitovu cha amani na kuvutia wawekezaji
Mwisho RC Chalamila amezungumzia suala la magari kupaki kwenye hifadhi za barabara yaani road reserve ambapo amesema hilo ni kosa kisheria hivyo ameitaka TANROAD kushughulikia ili hifadhi za barabara zisitumike vibaya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa