- Apongeza Manispaa ya Temeke na Kigamboni kwa kupata hati safi mwaka wa fedha 2021/2022
-Awataka kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 22,2023 amehitimisha ziara yake ya kushiriki *vikao vya kikanuni vya mabaraza ya kupitia hoja za CAG katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amezitaka Halmashauri hizo kupitia Wakurugenzi wake kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wanaohusika na upotevu wa fedha za umma.
Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa vikao hivyo katika *Manispaa ya Temeke na kuhitimisha Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
RC Chalamila amepongeza Manispaa hizo kwa kupata hati safi kufuatia ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG ya mwaka wa fedha 2021/2022 vilevile Ofisi ya CAG kupitia Ukaguzi wa Hesabu uliofanywa uliopekelea kubaini kasoro mbalimbali ambazo zinafanyiwa kazi na Halmashauri kwa masilahi mapana ya Umma
Aidha Mhe Chalamila amesema lazima Halmashauri zisimamie vizuri ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi ya fedha katika maeneo yao, pia kufanya kaguzi za mara kwa mara, kuongeza juhudi katika kuzuia hoja za CAG, usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, manunuzi ya Umma, kuhakikisha Mikopo iliyotolewa ya asilimia 10 inarejeshwa, kuboresha masoko ili kuongeza mapato na kuitumia vizuri Ofisi ya mkaguzi wa ndani
Hata hivyo RC Chalamila amewataka madiwani kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mkataba wa uendelezaji na Ubia wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kuonyesha tija ya mkataba huo kwa umma na dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuepuka upotoshwaji unaofanywa na watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania
Sambamba na hilo Mhe Chalamila amesema anatarajia kufanya ziara katika Wilaya zote za mkoa huo kwa lengo la kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusikiliza kero za wananchi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa