-Amshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
-Atoa rai kwa wananchi hususani wakazi wa DSM kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila mapema leo Agosti 23 ameungana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika matembezi ya hiari maarufu kwa jina la Tembea na Jakaya Kikwete Cardiac Institute.
Matembezi hayo ni muendelezo wa matukio mbalimbali kwa Taasisi hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya JKCI toka ianzishwe.
RC Chalamila akiongea baada ya matembezi hayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya hapa nchini hususani JKCI ambapo amesema uwekezaji katika Taasisi za afya ili uwe na tija lazima mambo muhimu zaidi ya matatu yazingatiwe mosi, Human Capital yaani wataalamu wa kutosha wenye sifa, pili Vifaa tiba vinavyoendana na Teknolojia ya kisasa, na tatu miundombinu mbinu safi kama vile majengo toshelevu.
"Ninamshukuru Mhe Rais kwa kuwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete mambo hayo yamezingatiwa ndiyo maana Taasisi hiyo imekuwa ikitoa huduma bora za kibobevu kwa watanzania na pia mataifa mengine ya nje na nchi jirani" Amesema Chalamila.
Aidha kuelekea maadhimisho ya miaka 10 JKCI imeendelea kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma kwa sasa tayari imeanzisha kitengo maalum cha Sports Cardiology ambacho kinatoa huduma ya Afya check kwa wanaofanya mazoezi na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu.
Mwisho RC Chalamila ameshiriki matembezi ya hiari kuanzia viwanja vya Farasi Ostytebay hadi JKCI makao makuu ambapo ameendelea kutoa rai kwa jamii umuhimu wa kushiriki mazoezi, kwa kuwa mazoezi ni Afya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa